Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwanafunzi wa miaka 17 mkoani Singida mbaroni kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa miaka minne.

 

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha), juu ya mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Chief Senge, kukamatwa kwa tuhuma ya kulawiti mtoto wa kiume wa miaka minne. (Picha na Nathaniel Limu).
******
Na Nathaniel Limu.
Jeshi la polisi mkoa wa Singida linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Chief Senge mjini Singida Ibrahimu Saidi (17), kwa tuhuma ya kumwingilia kimwilia kinyume na maumbile (kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne (jina tunalo).

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili 11 mwaka huu saa 11.30 jioni katika mtaa wa Majengo manispaa ya Singida.
Amesema mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa manispaa ya Singida, amepanga nyumba moja na wazazi wa mwaathirika/mlalamikaji.
Kamanda Kamwela amesema mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama alikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwa manafunzi huyo na hakukuwa na matatizo.
Amesema siku ya tukio, kama kawaida alipomwona mwanafunzi anaingia chumbani kwake, mtoto huyo naye alimfuata na kuingia chumbani humo.
Kamwela amesema mtoto huyo baada ya kuingia chumbani kwa mwanafunzi, mwanafunzi huyo alitumia fursa hiyo kumfanyia kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali.
Amesema hivi sasa wanakamilisha uchunguzi ili waweze kumfikisha mahakamani mwanafunzi huyo ili kwenda kujibu shitaka linalomkabili.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo Agnes Paulo, amesema siku ya tukio akiwa amepumuzika na wapangaji wengine, alimwona mtoto wake akitokea chumba cha mwanafunzi huko akilia kwa uchungu mkubwa.
“Nilipomuuliza, aliniambia kuwa Ibarahimu amemfanyia kitendo kibaya huku akionyesha kwa kidole sehemu yake ya siri ya nyuma.Baada ya kumchunguza,niliona damu zikimtoka kwenye hiyo sehemu ya siri”,alisema kwa masikitiko.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top