Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZIFF YAOMBA WA BONGO KUTUMA KAZI SIKU 2 ZILIZOBAKI

 


ZIFF waomba filamu za Bongo

UONGOZI  na  Wandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Film Festival (ZIFF) imesema kuwa imebakisha siku moja pekee kwa wasanii wa Tanzania na wale wa Afrika Mashariki kutuma kazi zao za filamu zitakazoingia kwenye  tuzo mbalimbali za  tamasha hilo linalotarajia kufanyika Juni 29 -Julai 7, mwaka huu.
 
Akizungumza na .... Mapema leo Meneja wa Tamasha hilo, Daniel Nyalusi alisema kuwa, toka ZIFF imeitisha upokeaji wa filamu kwa ajili ya Tamasha hilo la 16 la Nchi za Jahazi mnamo Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea Machi 31, 2013, hata hivyo kukawa na msukumo mdogo wa upokeaji wa filamu toka Tanzania, tofauti na nje ambapo mpaka sasa wameshapokea filamu zaidi ya 200 kwaajili ya uchaguzi wa jumla.
 
“Hii inasikitisha,  mpaka hatua ya mwisho wa zoezi la kupokea filamu za Kitanzania, ni filamu 5 tu ndio tulizopokea,  hivyo kuamua kuongeza muda hadi Aprili 15, tunaomba wasanii wa Tanzania na wa Afrika Mashariki kuchangamkia siku hizi mbili zilizobaki ilikutuma kazi zao” alisema Nyalusi.
Pia Nyalusi alisema kuwa, katika tamasha hilo ambalo mwaka huu linatimiza msimu wa 16, limesheheni mambo mbalimbali na kuwataka wadau kulisubili kwa hamu.
 
Aidha, Nyalusi alieleza kuwa,  kazi hizo za  Swahili Movie/Bongo Movie competition, ndizo filam zitakazotoa filamu Bora ya Kitanzania, filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine (Categories).
 
Hata hivyo, Nyalusi alitumia wasaha huo kwa wasanii wote kutuma kazi zao kwenye tovuti ya ziff ilikutuma kazi zao, ama katika ofisi zao za ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar.
 
Credits: Lukaza
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top