Kikosi
Kamili cha timu ya soka ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kikiwa katika
picha ya pamoja kabla ya mcherzo wa na Gymkhana jijini Dar es Salaam. Timu hizo
zilitoka sare ya mabao 3-3
Kikosi cha
timu ya soka ya Gymkhana.
Mshambuliaji
wa timu ya soka ya NSSF, Patrick Gandye akiwania mpira huku akizongwa na beki wa
timu ya Gymkhana, Hayssam Srour.
Clementi
Sanga akiambaa na mpira huku akifuatiliwa kwa karibu na mchezaji wa NSSF,
Kitwana Kidatu.
Kiungo wa
timu ya Gymkhana, Clement Sanga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga
akitafuta mbinu za kumtoka beki wa NSSF, Saleh Biboze wakati wa mchezo wa
kirafiki uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam.
DAR ES
SALAAM,Tanzania
TIMU ya
soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), juzi ilipigana kiume kutoka
nyuma kwa mabao 3-1 na kuambulia sare ya mabao 3-3 na Gymkhana FC, katika mechi
kali ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es
Salaam.
Ikicheza
kwenye dimba la nyumbani, Gymkhana FC ilimaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza
ikiwa mbele kwa mabao 3-1 yaliyowekwa nyavuni na mshambulia Radwan Kerdi
aliyefunga mara mbili na moja likitiwa kimiani na Erard Mutalemwa
‘Drogba.’
Bao la NSSF
katika dakika 45 za kwanza lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Nassor M. Nassor,
baada ya beki Linus Bwegoge aliyepanda kusaidia mashambuliazi kufanyiwa madhambi
ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru adhabu hiyo.
Kipindi cha
pili, NSSF walicharuka zaidi hasa baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha
mchezaji Khalid Jambia na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia nyota wake
Ahmed Hamisi ‘Kibela’ na Ali Chuo, hivyo kupata sare hiyo ya kuvutia ya
3-3.
Kocha wa
NSSF, Khalid Jambia alikiri kufurahishwa na upiganaji wa nyota wake, uliowezesha
kupata sare hiyo, iliyokuja baada ya mechi ya kwanza baina ya timu hizo
kuvunjika wakiwa hawajafungana, baada ya taa za uwanja huo
kuzimika.
Gymkhana FC
itabidi ijilaumu kwa kutoibuka na ushindi katika mechi hiyo iliyokuwa na nia ya
kuimarisha mahusiano mema baina ya Gymkhana - klabu inayohusisha michezo
mbalimbali na NSSF, baada ya kupoteza nafasi kadhaa kupitia nyota
wake.
Akizungumzia
mechi hiyo mchezaji wa Gymkhana, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga, alisema amekunwa na ushindani uliooneshwa, ingawa timu yake
ilikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi, kabla ya kuponzwa na kuridhika kwao na
uongozi wa 3-1.
“Nimeridhishwa
na ushindani na matokeo. Si kwamba hatukutaka kushinda, ila mabadiliko ya kikosi
chetu yalichangia, ingawa tumefanikisha lengo kuu la kuboresha mahusiano baina
ya Gymkhana na NSSF na kuchezesha kila mchezaji wa kikosi chetu,” alisema
Sanga.
Credits: Habari Mseto Blog



Post a Comment