SERIKALI ya Zanzibar , imesema inajiandaa kujenga
nyumba za makaazi kwa ajili ya askari wa Jeshi la Polisi, pamoja na vituo vya
kufanyia kazi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud
Mohammed, aliyasema hayo jan wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la
Muyuni jaaku Hashim Ayoub, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kujenga
nyumba hizo katika ukanda wa utalii.
Alisema nyumba na vituo vya kazi kwa
ajili ya askari Polisi tayari mradi huo upo ambao utekelezaji wake unafanywa kwa
pamoja na wafadhili, mbali mbali kwa kushirikiana na
wananchi.
Aidha, Waziri huyo alisema katika
kuutekeleza mpango huo, hivi sasa wameweza kujenga kituo cha Polisi cha Nungwi,
Kiwengwa na Paje ikiwa pamoja na kukamilisha ujenzi wa nyumba ya makaazi katika
eneo hilo la Paje.
Alisema kazi hiyo inaendelea
kufanyika katika kuyaangalia maeneo mengine ya ukanda wa utalii ili kuweza
kujenga nyumba hizo mpango ambao unaenda sambamaba na kuimrisha ulinzi wa Polisi
jamii.
Hata hivyo Waziri huyo, alisema
katika kukabiliana ana hali hiyo, pia serikali katika ukanda huo, imeweza kuunda
kikosi kazi cha ulinzi kwa ajili ya maeneo ya utalii kutokan ukanda wa pwani ya
Mashariki biashara hiyo imeimarika.
Kuna mabadiliko yameanza kufanyika
anakamilisha mfumo wa Baraza la Manispaa kwani likiyumba kidogo linaweza
kusababisha kutokea kwa matatizo.
Serikali
imeunda jopo la mawakili kupitia ripoti ya Kamati teule ya Baraza la Wawakilishi
juu ya utendaji wa Baraza la manispaa ili kuona namna ya kulifanyia kazi ambapo
hapo baadaea litafikishwa BLM Mawakili ambapo alisema imo katika hatua za mwisho
kusajili wageni
Post a Comment