Dk. Bitrina Dyamett akifungua mkutano uliowakutanisha wanasayansi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam.
Dk. Bitrina Dyamett akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Frorence Turuka, katika mkutano wa STIPRO.
****
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Nchi wa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetakiwa kuwa na ushirikiano mathubuti na Taasisi zinojihusisha na tafiti mbalimbali za kisayansi kama njia ya kuwasaidia wananchi wa nchi zao ili kujua matokeo ya tafiti zilizofanywa.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi utafiti ya STIPRO, Britrina Diyamett kwenye mkutano wa wadau wa tafiti za kisayansi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.
Amesema sehemu kubwa ya wananchi katika Jumuiya hii wamekuwa hawapati matokeo ya tafiti kwa wakati na hivyo kushindwa kuyatekeleza katika majukumu yao ya kimaendeleo.
“kuna mambo mengi ya kuyaangalia , kwanza tunaanza na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zishirikiane kwa kiasi kikubwa ili taarifa zetu za tafiti ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka,” amesema Diyamett.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dk Florens Turuka, alipongeza mpango wa mpadirishano wa sera za kitafiti ambao umewekwa na Taasisi hizo.
“ Hali hii inaonyesha kwa sasa watafiti wanaongezeka na hii itatusaidia kujidhatiti kutafuta majibu na njia za kufanya kutatua matatizo katika jamii,” amesema Dk. Turuka.
Post a Comment