Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWZZZZ...... MSAFARA WA MKUU WA WILAYA YA HANDENI MUHINGO RWEYEMAMU WAPAPATA AJALI,WAWILI WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE WAJERUHIWA VIBAYA.

DC RWEYEMAMU

Ajali hiyo imehusisha gari la Halmashauri ya wilaya ya Handeni ambapo watu wawili wamefariki akiwemo mwandishi wa Habari Hamis Bwanga na Afisa uhamiaji wa wilaya. 


Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 4.30 leo asubuhi katika kijiji cha Misima kweye barabara ya Handeni Korogwe wakiwa kwenye msafara wa kikazi kwenda vijijini kwaajili ya shughuli za upandaji wa miti kiwilaya. 

 

Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu amesema msafara huo ulikuwa na magari matatu ikiwemo ya kwake ambayo haijapata ajali.

 

Amesema gari hiyo ya halmashauri imepinduka baada ya kuacha njia na kwenda kama mita mia ambapo iliparamia jiwe na imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa maelezo yake taarifa zaidi zitapatikana baadae kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuwahudumia majeruhi ambao wanakimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro na pia kushughulikia miili ya marehemu.



 

Habari hii kwa hisani ya Vedasto Mwamsungu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top