Mamlaka ya SUMATRA imeaona faida ya kufanya kazi kwa pamoja katika usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini kwa kushirikiana kwa karibĂș sana na Jeshi la Polisi na Viongozi wa Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara.
Kama unavyofahamu, SUMATRA na Jeshi la Polisi tunashirikiana vyema katika maeneo kadhaa. Upande wa usafiri wa majini, tunashirikiana sana katika ulinzi na usalama kupitia Kikosi cha Polisi cha Wanamaji (Police Marine). Tupo pamoja pia katika Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Majini.
Katika eneo la usafiri wa reli, tunao Polisi wa Reli (Railway Police) katika TRL na TAZARA.
Kwa upande wa usafiri wa barabara tunacho Kikosi cha Usalama Barabarani. Ushirikiano wetu katika eneo hili ni wa kila siku na saa zote kutokana na ukweli kwamba usafiri wa njia ya barabara ni wenye kiwango cha chini cha usalama kuliko aina yoyote ya usafiri.
Aina hii ya usafiri inatugharimu rasilimali nyingi kwa maana ya fedha, watu na muda. Isitoshe aina hii ya usafiri inatumiwa na zaidi ya 80% ya watanzania kwa safari na bidhaa zao. Kwa mantiki hiyo basi ndiyo maana inatulazimu kuusimamia kwa karibu sana usafiri huu wa barabara.
Watanzania walio wengi wanatumia usafiri wa barabara katika shughuli zao za kila siku za kijamii na kiuchumi. Usafiri wa barabara hapa Tanzania na katika nchi nyingine zinazoendelea wanakabiliwa na matatizo mengi likiwemo hili la ajali za barabarani.
Pamoja na umuhimu wa usafiri wa barabara kwa jamii, lakini ni ukweli usipingika kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku ambapo mara nyingi husababishwa na makosa ya kibinadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri na hali ya miundombinu. Hali hii imekuwa ni kikwazo kikubwa katika juhudi za Serikali na wananchi kwa ujumla za kujiletea maendeleo.
Juhudi kadhaa zilikwisha chukuliwa katika kukabiliana na janga hili la ajali. Kutokana na ukweli huo, bado kuna umuhimu wa kuendelea na juhudi za kutafuta ufumbuzi wa kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la ajali.
SUMATRA kwa upande wetu tuliona ni vyema kuliangalia suala kwa undani zaidi ambapo Taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipewa jukumu la kufanya utafiti wa kina wa tatizo hili la ajali za barabarani katika Tanzania Bara.
Taarifa ya utafiti huo imedhihirisha kwamba ajali nyingi zinasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo ni uzembe wa madereva mwendo kasi, kuzidisha uzito, uchovu wa madereva, kutozingatia sheria/kanuni za usalama barabarani na ulevi. Makosa mengine yanahusiana na ubovu wa magari, matengenezo hafifu ya magari, mabasi kuundwa kwenye chesisi za malori na uchakavu wa magari. Hali ya barabara zetu nayo inachangia katika kusababisha ajali kutokana na kutokuwapo alama na ishara za barabarani, ubovu wa barabara, muundo wa barabara na hali ya hewa. Kwa kuangalia uwiano wa mchango wa kila sababu katika kusababisha ajali, imebainika kuwa makosa ya kibinadamu yanachangia 76% wakati hali ya gari inachangia kwa 16% na 8% inachangiwa na hali ya miundombinu ya barabara.
Ili kukabiliana na ongezeko la ajali za barabara watafiti walipendekeza pamoja na mambo mengine kwamba mamlaka husika kusimamia utekelezaji wa Sheria zilizopo za Usalama Barabarani, kuimarisha na kuboresha mafunzo kwa madereva wa magari ya abiria, kutoa elimu kwa watumiaji wote wa barabara, Sheria/kanuni zirekebishwe ili kulazimisha matumizi ya mikanda ya usalama katika magari na kofia za chuma kwa wapanda pikipiki na kuwepo na huduma za uokoaji katika matukio ya ajali. Mapendekezo mengini ni barabara kukarabatiwa kila kunapotokea uharibifu, ushirikiano kati ya vyombo vinavyohusika na usafiri na usalama wa barabara uimarishwe kuanzia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na SUMATRA na Jeshi la Polisi wasimamie viwango vya usalama katika mabasi ikiwa ni pamoja kuboresha usimamizi wa kanuni (regulations) zinazohusu madereva wa mabasi na kusimamia kwa ukaribu zaidi huduma zinazotolewa na kuwanyima liseni wakiukaji wa kanuni.
Kutokana na matokeo ya utafiti huo, ni matumaini yetu kuwa sisi kama wasimamizi wa usafiri tukifanya kazi kwa pamoja, kwa umakini na weledi tutaweza kutimiza malengo tuliyojipangia ya kupunguza .
Kama ilivyobainishwa katika utafiti iliyofanyika mwaka 2007 kuwa makosa ya kibinadamu yamechukua nafasi kubwa katika kusababisha ajali, Mamlaka imeonelea kuna haja ya kuimarisha shughuli za ufuatiliaji wa madereva ambao wamekuwa wakijihusisha na ulevi na kusabaisha ajali.
Kutokana na hali hiyo Mamlaka inatoa vifaa vya kupima ulevi kwa Kikosi cha Usalama Barabarani ili waweze kutumia katika kuwabaini madereva walevi ambao wamekuwa moja ya vyanzo vya ajali katika usafiri wa barabara.
Post a Comment