STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
19 April , 2013 ______________________________

__________
Ushiriki wa wananchi katika ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii
umeleta mafanikio katika kupunguza vitendo vya uhalifu nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame wakati akiwasilisha taarifa
ya Utekelezaji wa Mpangokazi Idara ya Uratibu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa katika Ofisi hiyo.
Dk. Mwinyihaji amesema katika kuimarisha ulinzi na usalama jumla ya
vikao 58 vya Kamati za Ulinzi na Usalama vimefanyika Unguja na Pemba
lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi na kuhamasisha wananchi kushiriki
zaidi katika ulinzi wao wenyewe na mali zao.
Kuhusu suala la mifugo inayozurura ovyo mijini kwa kuanzia amesema
operasheni maalum inaendelea katika Manispaa ya Zanzibar ambapo
Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa hadi sasa
wameshakamata mifugo 153 iliyokutwa ikizurura ovyo.
Kati ya mifugo hiyo alieleza ng’ombe 43, mbuzi 58 na punda mmoja
wameshakombolewa na Serikali imekusanya jumla ya shilingi milioni 4.3
ikiwa ni faini kutoka kwa wamiliki wake.
Katika taarifa yake Waziri Mwinyihaji ameeleza kazi ya kuung’arisha
mji wa Zanzibar inaendelea ambapo mradi wa majaribio kwa kuweka taa za
barabarani kwa kutumia umeme jua umeanza majaribio ambapo taa katika
baadhi ya mitaa ya Manispaa zimeanza kuwashwa.
Waziri aliongeza kuwa Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa
zinaendelea kuimarisha utoaji huduma mbalimbali kwa wananchi kwa
kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali zikiwemo afya, maji, elimu
na huduma za kiuchumi na biashara kama vile ujenzi na ukarabati wa
masoko na huduma zake kama sehemu za kufanyia biashara na vyoo.
Kikao hicho cha tathmini ya Mpangokazi ambacho kiko chini ya uenyekiti
wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kimehudhuriwa
pia na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad na Katibu
Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
Postal Address: 2422 Tel.:0776 613 015. Fax: 024 2231822
E-mail: saidameir@ikuluzanzibar.go.tz, sjka1960@hotmail.com

Post a Comment