
Ujumbe wa Kampuni ya Bia Tanzania unaoongozwa na
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (pili kulia) ukiingia kwenye
viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Mapema leo asubuhi kwa kuhudhuria Mkutano wa 11
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wengine pichani toka kulia ni
Mratibu wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya
Safari Lager,Innocent Melleck,Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia
Tanzania,Phocas Laswai,Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe,Mkuu wa Mauzo
wa Kanda ya Mashariki,James Bokela pamoja na Meneja Mauzo wa TBL,Kanda ya
Kati,Julius Ngaga.Ujumbe huu upo mjini Dodoma kwa azili ya kupata Baraka za
wabunge na uzinduzi rasmi wa Ziara ya Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika
ulioupata Bia ya Safari Lager,ambapo jioni ya leo kutakuwa na tafrija fupi ya
kupongeza ushindi huo itakayofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini
Dodoma.

Wakijadiliana jambo kabla ya kuingia kwenye
ukumbi wa Bunge ili kufatilia shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na
Bunge.

Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge kufatilia
shunghuli mbali mbali zinazoendeshwa na Bunge.


Post a Comment