Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UFAFANUZI KUHUSU SERIKALI KUWAPATIA WANANCHI SEHEMU KUBWA YA ENEO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO


SONY DSCWAZIRIWIZARA YA MALIASILI NA UTALII Mhe. Balozi Khamis Kagasheki akitoa ufafanuzi kuhusu eneo la pori TENGEFU LA LOLIONDO Kwa waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMONWA FULLSHANGWE )
********
SERIKALI inasikitishwa na baadhi ya Asasi za kirai na vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli kuhusu mgogoro wa ardhi katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Kagasheki amesema kuwa eneo la pori tengefu la Loliondo ni miliki halali ya serikali kwa mujibu wa sheria ya umilikaji ardhi tokea kabla na baada ya ukoloni.Historia inaonyesha kuwa mwaka 1902 utawala wa ujerumani walitunga sheria ya umiliki na matumizi ya ardhi ambapo ardhi ilibaki kuwa chini ya serikali,vivyo hivyo kwa utawala wa Waingereza mnamo mwaka 1923 na 1974 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro huo Kagasheki amesema kuwa kinachofanyika sasa ni Serikali kumega ardhi yake na kuwapatia wananchi na si kama inavyoripotiwa na vyombo vingi vya habari.

“Ndugu waandishi siyo sahihi kwa baadhi ya NGO’s kusema kuwa Serikali imenyakua ardhi kutoka kwa wananchi,ukweli ni kuwa Serikali ndiyo iliyomega ardhi yake na kuwapatia wananchi,yaani kilometa za mraba 2500 sawa na asilimia 62.7 ya eneo zima la pori tengefu la Loliondo” Alisema Kagasheki.
Aidha aliongeza kuwa kutokana na makosa yaliyofanyika huko nyuma ya kuwapati wananchi hati ya kinyume na utaratibu na kuwaaminisha wananchi uhalali wa kumiliki eneo lote la pori tengefu,Serikali kwa kuthamini wananchi wake imeamua kutenga eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2500 kwa ajili ya vijiji ili wananchi wawe wamiliki halali na kwa mujibu wa sheria tofauti na ilivyo sasa.
Hata hivyo alisema kuwa eneo lililo baki ndiyo litakuwa hifadhi ya pori tengefu ambapo litakabidhiwa kwa mamlaka za hifadhi za taifa.
Eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4000 liligeuzwa kuwa pori tengefu la Loliondo mnamo mwaka 1974 baada ya serikali kupitia Wizara yake ya Maliasili na Utalii,kutangaza kwa tangazo namba 269 katika gazeti la Serikali.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top