Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakaguzi wa ndani wapigwa msasa

 

1
 
Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Constantine Mashoko (kulia) akifungua kikao kazi kwa Wakaguzi wa Ndani wa Sekretarieti za mikoa Tanzania bara jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi –Technical Audit – Amin Mcharo. Kikao hicho kilenga kutathmini jukumu la wakaguzi wa ndani. 2
 
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Ndani wakiandika mambo muhmu wakati wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikalii Constantine Mashoko (hayupo pichani) akifungua kikao kazi kwa Wakaguzi wa Ndani wa Sekretarieti za mikoa Tanzania bara jana jijini Dar es salaam 2A
 
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Ndani wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikalii Constantine Mashoko (hayupo pichani) akifungua kikao kazi kwa Wakaguzi wa Ndani wa Sekretarieti za mikoa Tanzania bara jana jijini Dar es salaam PAMOJA
 
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Ndani wakiwa katika pamoja na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikalii Constantine Mashoko baada ya kufungua kikao kazi kwa Wakaguzi wa Ndani wa Sekretarieti za mikoa Tanzania bara jana jijini Dar es salaam.
Picha na MAELEZO_DAR ES SALAAM

……………………………………………………………
Na MAELEZO-DAR ES SALAAM
IDARA ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali imewaagiza Wakaguzi wote wa ndani kusimamia vema matumizi ya rasilimali za umma ili matokeo ya usimamizi mzuri yalete matunda mazuri kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana jana na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Constantine Mashoko wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu cha Wakaguzi wa Ndani wa Sekretarieti za mikoa Tanzania bara kilicholenga kutathmini jukumu la wakaguzi wa ndani.
Alisema kuwa wakaguzi wa Ndani wa Serikali wanalojukumu la kuhakikisha kuwa rasilimali za ummazinatumika kama ilivyokusudiwa kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Mashoko alioneza kuwa wanalojukumu la kuhakikisha kuwa ukaguzi unafanyika kikamilifu katika maeneo yao ya kazi ili kuwezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali aliwaasa wakaguzi hao kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kuogopa mabadiliko na hivyo kutoisaidia Serikali katika kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mashoko aliongeza kuwa ni vema wakaguzi wa ndani wakawa waadilifu ili waweze kutoa taarifa zenye hisia za ubadhirifu kikamilifu na kuepuka vitendo ambavyo havikubaliki kulingana na maadili ya taaluma yao.
Alisema kuwa Serikali haitasita kuwaondoa kwenye nafasi zao wale wote watakaobainika kwenda kinyume na maadili ambapo lengo ni kuhakikisha kuwa kazi ya ukaguzi wa ndani inakuwa na tija kwa Serikali na wanachi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top