Maandalizi kwa ajili ya zoezi la usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama cha Netiboli Tanzania CHANETA utakaofanyika aprili 20 mwaka huu mjini Dodoma yamekamilika na kinachosubiriwa ni wajumbe wote kuwasili na mpaka sasa wajumbe wengi wameshawasili mjini humo na wengine wapo njiani.
Akizungumza na FULLSHANGWE kutoka mjini Dodoma Kaimu katibu mkuu wa CHANETA Rose Mkisi alisema kesho saa mbili asubuhi zoezi linaanza rasimi huku kila mjumbe aliyechukua fomu ya kugombea akipangiwa muda wake.
“Tunatarajia zoezi liendeshwa kwa haki, kila mgombea atasailiwa kulingana na kanuni zilizowekwa na chama hicho, atakayefuzu vigezo utapita na kama mtu hatakidhi vigezo basi kutakuwa hakuna jinsi kwa kweli”. Alisema Mkisi.
Mkisi aliongeza kuwa kesho kutwa aprili 19 kutakuwa na nafasi ya wagombe kuweka pingamizi au kupinga maamuzi yatayotolewa na kamati ya uchaguzi.
“Kama kuna mtu hataridhika na maamuzi juu yake, ana nafasi keshokutwa kuwasilisha pingamizi lake, haki itatendeka na hakuna mtu atakayeondolewa akiwa na kigezo”. Alisisitiza Mkisi.
Katibu huyo alisema kuwa aprili 20 asubuhi kutakuwa na mkutano mkuu wa Uchaguzi ambapo uongozi wa CHANETA utatoa taarifa zake na baada ya hapo utajiuzulu na kukabidhi madaraka kwa kamati ya uchaguzi tayari kwa kuwapata vongozi wapya.
“Naomba kusisitiza kuwa hakutakuwa na Mkutano mkuu wa chama kwasababu ulishafanyika wakati wa mabadiliko ya katiba, siku hiyo kutakuwa na mkutano mkuu wa Uchaguzi, naomba nieleweke”. Alifafanua Mkisi.
Mkisi aliwataka watanzania kuamini kuwa CHANETA imejipanga kuendesha uchaguzi wa huru na haki na mtu atapita kwa kura za wajumbe na si vinginevyo.
(Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam)
Post a Comment