Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule kwa pamoja na Bibi Petra Hammelmann,
Mwakilishi wa Heshima Mteule wa Tanzania mjini Hamburg nchiniUjerumani wakisaini
Mkataba wa kumwezesha Bibi Hammelmann kuwa Mwakilishi wa Heshima rasmi wa
Tanzania katika mji huo. Mkataba huo ulisainiwa Wizarani tarehe 16 Aprili,
2013.
Bw. Haule na Bibi Hammelmann wakibadilishana
mkataba huo mara baada ya kusaini.
Bw. Haule akizungumza na Bibi
Hammelmann mara baada ya kusaini mkataba utakaomwezesha Bibi Hammelmann kuwa
Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania mjini Hamburg. Pamoja na mambo mengine Bw.
Haule alimhimiza Mwakilishi huyo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania mjini
Hamburg ili kukuza sekta ya utalii hapa nchini.
Bw. Haule akiendelea na mazungumzo na Bibi
Hammelmann huku Bw. Mwandembwa na Bw. Ali wakisikiliza.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bw. Andy Mwandembwa (kushoto) pamoja na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya
Nje kutoka Kitengo cha Sheria wakishuhudia uwekaji saini huo.Picha na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa
Post a Comment