Mwenyekiti wa kundi la wake wa mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni akifungua mkutano wa wake wa mabalozi nchini “Coffee meeting” uliyofanyika katika ukumbi wa Synergy Grill Oysterbay jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Mke wa Balozi wa Japani nchini Tanzania Bi. Keiko Okada (kulia) akimtambulisha aliyewahi kuwa Miss Tanzania (2008) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Duka la bidhaa za Kiutamaduni zinazotengenezwa kwa Mikono na wanawake wa Kimasai – ENJIPAI Nasreen Karim aliyepata fursa ya kuonyesha kazi za mikono zinazotengenezwa na wanawake wa Kimasai walioko katika kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim (wa pili kulia) lilipo barabara ya Kaunda Drive Oysterbay jijini Dar es Salaam akielezea namna anavyofanya kazi zake za ubunifu wa bidhaa za shanga na kinamama wa Kimasai.
Sehemu ya wake wa Mabalozi nchini na wageni waalikwa wakipiga makofi baada ya kusikia Utambulisho wa kazi anazofanya Nasreen Karim Mkurugenzi Mkuu wa Duka la ENJIPAI.
Picha juu na chini wake wa mabalozi nchini katika Coffee meeting yao.
Nasreen Karim akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa kutoka Umoja wa Ulaya.
Nasreen Karim akimvisha moja ya bidhaa za Shanga mmoja wa wageni waalikwa kutoka World Bank Bi. Sharon Mitchell aliyetokea kuvutiwa na kazi za mikono ya kinamama wa Kimasai wa duka la ENJIPAI.
Mkurugenzi Mkuu wa Duka la ENJIPAI Nasreen Karim akimvisha mkufu wa shanga mmoja wa wake wa mabalozi wakati wa maonyesho ya bidhaa zake kwenye Coffee meeting ya wake wa mabalozi nchini.
Mke wa Balozi wa Nigeria Bi. Naomi Majnabu (kushoto) na Mke wa Balozi wa Rwanda nchini Bi. Mary Rugangazi (katikati) wakimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim kwa kazi nzuri ya ujasiriamali anayofanya.
Nasreen Karim akifurahi jambo na Mke wa Balozi wa Misri wakati wa maonyesho ya bidhaa za duka la ENJIPAI yakiendelea.
Nasreen Karim katika picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim katika picha ya pamoja na baadhi ya kinamama wa Kimasai anaofanya nao kazi za kutengeneza bidhaa za shanga mara baada ya maonyesho hayo wakati wa Coffee meeting ya wake wa mabalozi.
Na. Mwandishi wetu
Wanawake wajasiria mali haswa wa fani ya vifaa vya urembo vya asili kama vile mikufu ya shanga na vinginevyo nchini Tanzania wametakiwa kujitangaza zaidi kimataifa kwa kushiriki maonyesho mbalimbali ili kuonyesha uwezo wao.
Akitoa rai hiyo wakati akimtambulisha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya inayotengeneza bidhaa hizo ya Enjipai Bi. Nasreen Karim kwa niaba ya wake wa mabalozi hao, Mke wa Balozi wa Japan hapa Tanzania Keiko Okada amesema bidhaa hizo zinazo tengenezwa kwa shanga zinapendwa na zinahitaji kutangazwa kimataifa.
Wake wa mabalozi hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mikutano yao ya kila mwezi maarufu kama ‘Coffe Meeting’, kuzungumzia miradi wanayoifanya ambapo kila wakati huwa wanaalika wajasiria mali tofauti na kwa wakati huu wamealika kampuni iliyokusanya akimama wa kimasai wanaotengeneza bidhaa tofauti za shanga ya’Enjipai’.
Enjipai ni kikundi kilichoanzishwa miaka miwili iliyopita chini ya Bi. Nasreen Karim na leo kupata mualiko kutoka kwa wake za mabalozi kuonyesha bidhaa wanazozitengeneza..
Akizungumza Mimi niko Nasreen Karim kama unavyojua kazi zetu ni kwa wawezesha wanawake kwa namna hiyo hivyo nitazungumza na wageni hawa kuwaonyesha bidhaa zetu na baadae tukimaliza watatambua wapi tunataka kuelekea na kudhibitisha kuwa tukiwezeshwa tunaweza.
Post a Comment