Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

wanahabari wapewa mafunzo kuhusu ripoti ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012


picha no. 1
 
Mratibu wa Sensa Zanzibar, Mayasa Mwinyi (kushoto) akimuelekeza mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Darlin Said (kulia) jinsi ya kutumia takwimu za sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala , matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. picha no. 2
 
Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Ephraim Kwesigabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kuripoti kwa usahihi taarifa ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam.
picha no. 4
 
Waandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally (kushoto) na Mohamed Mohamed (kulia) wakisoma ripoti ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. NBS iliandaa mafunzo hayo ya siku moja ili vyombo vya habari viweze kuripoti kwa usahihi taarifa ya sensa. picha no. 6
 
Mchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ariv Severe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kutumia tovuti ya NBS ambayo inataarifa mbalimbali ikiwemo ya ripoti ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. picha no.3
 
Mhariri wa Habari Msaidizi Stella Nyemenohi kutoka gazeti la Habarileo akitoa maoni yake jinsi waandishi wa habari wanavyoweza kutumia ripoti ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 kupata majibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na totauti ya idadi ya watu kati ya mkoa mmoja na mwingine wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mpiga picha wa kampuni ya New habari (2006) Anthony Siame na kulia ni mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally.
picha no.7
 
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Irenius Ruyobya (kushoto) akiongea jambo na mtaalamu wa mawasiliano ya umma Said Ameir wote kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu jinsi ya kutumia takwimu za sensa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. picha no.8
 
 
credits: FullshangweBlog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top