Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANAKIJIJI WA CHAMWINO WALIA NA NJAA


VIJIJI vyote 77 vya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma vimekumbwa na baa la njaa kutokana na ukame mkali uliodumu kwa miezi miwili mfurulizo.
Ukame huo ulio ulioanza mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mpaka mwishoni mwa mwezi wa pili umefanya hali ya chakula kuwa mbaya Wilayani humo hali inayozidi kutishia maisha ya watu.
Akitoa taarifa ya hali ya chakula Afsa kilimo wa Wilaya ya
Chamwino kwenye Baraza la Madiwani lililofanyika jana Gofrey Mnyamale alisema kutonyesha Mvua kwa kipindi hicho kumesababisha hata zao la Mtama ambalo huwa linastahimili ukame kukauka.
Alisema katika msimu wa kilimo wa Mwaka 2012/13 wilaya ilijiwekea malengo ya kulima Hekta 118, 071 za mazao ya chakula na kutarajia kuvuna tani 105, 040 kama Mtama, Mahindi na uwele lakini malengo hayo yamepotea.
Aliongeza kuwa Mvua nyingi zililizonyesha katika mtiririko usioridhisha hasa Mwezi Desemba na kufuatia na ukame mkali katika miezi hiyo miwili kuliwapoteza watu waliozoea kupanda mapema kutokana na hali ya hewa ya mkoa wenyewe.

Mnyamale alitanabaisha kuwa waliamua kuwaagiza wananchi kutunza chakula kidogo walichonacho, wenye mifugo kuuza ili kununua chakula, kuzuia wafanyabiashara wasitoe nje chakula na kufanya tasmini ya kina ili taarifa ipelekwe kwa Waziri mkuu mapema iwezekanavyo.
‘’Tunataka baada ya kukamilisha Tathimini hii Taarifa itapelekwa haraka kwa Waziri Mkuu ili hatua za haraka za kunusuru watu dhidi ya janga la njaa zichukuliwe mapema mapema iwezekanavyo ambapo tunatarajia kabla Mei 10 mwaka huu kuwa imekamilika’’, alisema
Kwa upande wake Mjumbe wa NEC ya CCM Samwel Malecela aliitaka Selekari kuchukua hatua za Halaka ili kunusuru hali ya njaa katika Wilaya nyingi kutokana na upungufu wa chakula kuwa kila sehemu.
‘’ Janga hili ni kubwa na Mala nyingi Selekari imekuwa ikisema inafanya upembuzi yakinifu na inatumia muda mwingi kupembua katika hili nawaambia wafanye haraka kwani hali ni mbaya mno bora kitu kingine kuliko njaa’’, alisema
Malecela Aliongeza kuwa yeye kwa nafasi yake anatembea kila wilaya na amebakiza chache ili amalize na sehemu kubwa inatatizo la kukosa chakula hivyo serekali ihakikishe inatoa kipaumbele kuanzia na wilaya zilizoathirika sana kama hiyo ya Chamwino anakotokea.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top