Kwa
mujibu wa utafiti huo uliofanywa katika
nchi 14 ikiwamo Tanzania
katika kipindi cha miaka 16 iliyopita kuanzia mwaka 1995 hadi 2011, watu wengi
wamekuwa wakifanya makosa kwa namna mbalimbali katika kutumia kandomu ikiwamo
uvaaji.
“Makosa yanayofanywa mara kwa mara na watumiaji wa
kondomu ni pamoja na kuingiza kinga hiyo nusu katika uume wakati wa ngono au
kuitoa kabla tendo hilo halijamalizika au kusubiri mpaka isinyae,” imesema
sehemu ya utafiti huo.
Makosa mengine ni kutoacha nafasi katika ncha ya
kondomu kwa ajili ya mbegu za kiume na kuzifungua vibaya katika pakiti
yake.
on Saturday, April 20, 2013



Post a Comment