'Lisemwalo
lipo, kama halipo liko njiani linakuja’
KAMA si
Menejimenti ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital), basi Serikali
yenyewe kwa ujumla wake, ikomeshe tuhuma za kuwepo rushwa kwa Wajawazito
wanaojifungua, na Wizi wa watoto wachanga wakati wa upasuaji; Jambo ambalo
linaitia aibu Hospitali hiyo na Taifa.
Wajawazito
walio wengi na wazazi waliojifungua salama hospitalini hapo na kuomba wasitajwe,
wamelalamikia kuwepo kwa rushwa iliyokithiri wanapojifungua, ikidaiwa wanombwa
kutoa kati ya Sh.60,000 – 300,000/- kulingana na ukubwa wa
tatizo; na
wanaojifungua kwa upasuaji, wamekuwa wakiibiwa watoto au kubadilishiwa
waliokufa.
Kashfa kama
hiyo na nyinginezo, awali iliiandama sana Hospitali ya Mwanyamala Dar es salaam,
lakini sasa meota na kumea Dodoma, vilipo vikao vya Bunge, jambo ambalo ni aibu
kwa Menejimenti ya Hospitali hiyo, Watalaam, Watendaji na Serikali nzima kwa
ujumla.
Jumatano,
Aprili 17, mwaka huu, Amana Amosi Mbigili na Mumewe Isaya Nyembele, walionja
Uchungu wa Uzazi ambapo baada ya Amana kujaliwa mtoto kwa upasuaji, alifanyiwa
njama abadilishiwe mtoto liyekufa, ambapo kwa ujasiri Amana aling’ang’ana kuwa
arudishiwe mwanae hai aliyebebwa na Muuguzi.
Pamoja na
Kaimu Mganga Mkuu Zainab Chaula kukiri ni kweli tukio hilo lilitokea lakini
limenukuliwa tofauti, kwa nini nduguze wpelekwe chumba cha maiti wakakabidhiwe
mtoto aliyekufa? Kwa nini mtoto awekwe mbali na Mzazi wake? Kwa nini mtoto
apatikane baada ya malumbano ya wazazi kutishia
kumuona Mganga Mkuu wa Mkoa?
Bado tuna
kumbukumbu miaka ya nyuma, ambapo Hospitali hii ilikumbwa na Kashfa ya kuwa na
Dakitari aliyekuwa na vyeti na, Serikali ikamuajiri akalipwa Kodi ya
walalahoi.
Bado
hatujasahau walala hai waliposababisha watalaam Mhimbili walimfanyie mtu
upasuaji wa kichwa badala ya mguu. Ndiyo maana tunasikiti na kulia tunapoona
Kiti cha Spika na Serikali Sikivu, vinawasikia na kuwakumbatia baadhi ya Wabunge
wavuta Bangi wanaotukana Matusi bungeni, wakati mashamba ya Bange yanatomwa, ni
Jinai.
Kwa ufupi
kilichomtokea Amana aliyefanyiwa upasuaji akiwa kitandani alidai
hivi,
“Nlishangazwa
na kitendo cha Muuguzi kunilaza chumba tofauti na mwanangu; nilipomuuliza mtoto
akanijibu alishafariki, kitendo ambacho sikuridhika nacho, kutokana na kuona
mtoto mwingine akipitishwa na kuingizwa chumba kingine akiwa amefungwa na nguo
nilizofika nazo hospitalini akiwa hai.
“Nilikuwa
hoi na maumivu makali, lakini nilikuwa na ufahamu. Nilipoanza kulalamika kwa
sauti, ndipo wakaamua kuniletea mtoto wangu akiwa hai, kitendo kilichonifanya
nilie kwa furaha baada ya kumpata mwanangu. Si kweli kwamba walichanganya
watoto, walitaka kuniibia makusudi.
Kama
walichanganya watoto, mbona sikumuona mama wa mtoto marehemu? Mungu ndiye
anajua, mimi namshukuru,’’ alisema Amana.
“Hawawezi
kuniuliza lolote! Hebu hilo liwe funz kwaoo, lakini ni vema Serikali ikomesha
madhaifu haya, maana yanaitia aibu Taifa na viongozi wake. Mke wangu bado ana
maumivu makali, hivyo tunaendelea kumuuguzi na bado amelazwa kama unavyoona, na
mimi sichezi mbali”.alisema Nyembele.
Mganga Mkuu
wa Mkoa Dkt. Ezekiel Mpuya ambaye hakuwepo siku hiyo alipohojiwa na Mwandishi
alikiri kusikia Malalamiko hayo na atayafanyia kazi ikiwa ni pamoja na
kufuatilia kwa karibu tuhuma ya rushwa iliyokithiri kwa wajawazito wakati wa
kujifungua, ili wachukuliwa hatua Kali.
Ni rai
yangu Hospitali ya Dodoma ikomeshe
Rushwa na Wizi wa Watoto Wachanga.
(Na Bryceson Mathias wa Habari Mseto blog)



Post a Comment