Bw.Mizengo
Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania |
Waziri Mkuu wa Tanzania
Bw.Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili
kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka
2050.
Akizindua ripoti ya
idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia, wiki hii jijini
Dar es Salaam, Waziri Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama
ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka
2006.
Alisema ni vyema
Watanzania wakaachana na dhana potofu kuwa kuzaa watoto wengi ni umaarufu na
utajiri.
Desemba 31, mwaka jana,
Rais Jakaya Kikwete alizindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2012
ambapo idadi ya Watanzania ilifikia milioni
44.9.
Matokeo hayo yalionyesha
kuwa wanawake ni asilimia 51 wakati wanaume ni asilimia
49.
Kimkoa, ripoti hiyo
ilionyesha mikoa yenye idadi kubwa ya watu kuwa ni Dar es Salaam wenye idadi ya
watu Milioni 4,364,541. Mwanza 2, 727, 509 na Mbeya
2,707,410.
Pinda alisema, Serikali
itaendelea kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango
kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya
watu.
Vilevile Pinda alisema
iwapo ongezeko la watu la asilimia 2.7 kwa mwaka litaendelea basi idadi ya watu
Tanzania itafikia milioni 90 ifikapo mwaka
2050.
Ripoti hiyo ilionyesha
kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una ongezeko kubwa la watu kwa asilimia 5.6 kwa mwaka
ukifuatiwa na Mkoa wa Mjini Magharibi na Unguja ambapo kasi katika miji hiyo ni
asilimia 4.2.
Alisema msongamano wa
watu katika miji hiyo ni mkubwa na unasababisha shinikizo katika utoaji wa
huduma za maendeleo kama maji, elimu, afya, umeme na
miundombinu.
Post a Comment