Yanga
ambayo inafukuzia taji la Ligi Kuu ya Tanzania Baraleo itashuka dimbani
kupambana na JKT Ruvu ya mkoani Pwani kwenye mchezo utakaochezwa uwanja wa
Taifa.
Yanga
ambao ni wenyeji katika mchezo huo watahitaji kupata pointi zote tatu ili kuweka
matumaini makubwa ya kuchukua Ubingwa wa bara.
Pia JKT
Ruvu nao watahitaji kupata matokeo mazuri ili kujinasua kwenye mstari wa
kushuka daraja kwani hawako katika nafasi nzuri.
Timu ya
Yanga imejipanga vema kufanya kweli kwani wakifanikiwa kupata pointi zote
kutawafanya wahitaji sare moja tu ili kutangaza ubingwa.


Post a Comment