Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakati Maduro akiapishwa kuwa rais mpya wa Venezuela avamiwa na kunyang’anywa kipaza sauti na mtu asiejulikana.

Mwanasiasa Nicolas Maduro ameapishwa rasmi kuwa rais wa Venezuela na kuchukua nafasi ya Hugo Chavez.
Akizungumza baada ya kuapishwa Maduro ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na upinzani ili kuijenga nchi yao iwe bora zaidi.
Maduro mwenye umri wa miaka 50 amesema anataka kuanza kipindi chake cha urais kwa kuwataka watu wa Venezuela kuijenga nchi hiyo iwe ya amani.
Hata hivyo, wakati akihutubia mbele ya marais, mawaziri wakuu na viongozi wengine, hotuba hiyo ilivurugwa baada ya mtu mmoja kuvamia jukwaa na kumpokonya kipaza sauti.
Akizungumza baada ya tukio hilo lililoleta mkanganyiko, Maduro ameisema vikosi vya usalama vimeshindwa kazi, kwani angeweza kuuawa.
Maduro ameapishwa saa chache baada ya tume ya uchaguzi ya Venezuela kusema itahesabu tena kura zilizosalia za uchaguzi wa Jumapili iliyopita kufuatia mpinzani wake Henrique Capriles, kudai kura zihesabiwe upya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top