
Mkutano wa Mawaziri wa Baraza la Amani na Usalama la
Umoja wa Afrika (AU) utafanyika hapa Dar Es Salaam tarehe 22 Aprili, 2013.
Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika lina wajumbe 15 kutoka kwenye Kanda zote tano za
Umoja wa Afrika. Wajumbe hao ni Algeria, Angola, Cameroon, Congo (Barazzaville),
Cote d’Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Gambia, Guinea, Lesotho, Misri,
Msumbiji, Nigeria Uganda na Tanzania.
Baraza hilo
litakalokutana chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe, litajadili pamoja na mambo mengine,
hali ya kisiasa nchini Madagascar ambayo iliathiriwa vibaya na mapinduzi
yaliyofanyika nchini humo mwezi Machi, 2009.
4Mkutano huo muhimu unatarajiwa kupendekeza mikakati ya
kusaidia Madagascar kufanya uchaguzi huru na wa haki mwezi Julai, 2013.
IMETOLEWA NA WIZARA
YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA
KIMATAIFA, DAR ES
SALAAM.
20 APRILI 2013


Post a Comment