Mbunge wa Arusha Mjini kupitia chama cha Demokrasia ma Maendeleo (CHADEMA) Ndugu "Godbless Lema" usiku wa jana kuamkia leo saa8 amefikishwa Central Police bila kufahamika chanzo... Hii inatupa wasiwasi na kubaini kua kuna mchezo nyuma ya pazia unaochezwa na kundi la watu wa chache katika siasa upande wa pili wa upinzani kibaya zaidi ni ma'askari waliovamilia nyumbani kwa mbunge usiku wa jana na kulipua mabomu na wakiwa na silaha kali utadhani wamekwenda kumkamata jambazi au mtu mwenye kesi ya mauaji kitu ambacho sio kizuri. #Pole kwa familia ya Godbless Lema.
JOSHUA NASSARI - MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI:
Nimepata kwa mshtuko na
nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira
nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.
Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye
dhamana ya kusaidia kuilinda kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa
wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema
achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti
mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi
usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni
arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani,
kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
Nyumbani kwa mbunge hakai mbunge mwenyewe.
Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke, ndugu etc. Utapigaje
mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa mauaji. Lema si jambazi, ni
kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana na mzalendo kwa taifa
lake.
Hii
wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological
tortue.
Kama
amenielewa atasikia, otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na
tulishakuwa tayari, hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani
arusha juni 16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu
ya mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa mgumu,
ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"
Nassari.
MKE WA GODBLESS LEMA
Taarifa za sasa kutoka
Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na
jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za
Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha
juzi.
Taarifa za uhakika
kutoka kwa mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana
yake na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.
Namkariri Mke wa Lema
akiongea akisema “jana usiku saa sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani
kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni
Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli
au ni watu wanataka kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi
kutwa nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”
“Baada ya muda kusogea ikabidi Lema aanze
kuwapigia marafiki, jamaa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya hapo pia
tuliamua kupiga kengele ya kampuni ya security ambao muda mfupi baadae walikuja
na gari yao huku Polisi wakiendelea na vitisho kwamba watapiga mabomu na kuvunja
ukuta la sivyo Lema ajisalimishe, Viongozi wa Chadema na marafiki walipowasili
wakamshauri Lema ndio akajitokeza wakati huo ni saa tisa usiku” – Mama
Lema
“Alipojitokeza Polisi
walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa
maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa
rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye
kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa
nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika
jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama
Lema
“shitaka kubwa lililo
mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo
cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo
Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote
ni uoga” – Mama Lema
Kwa kumalizia, Mke wa
Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa
baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa…………
toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake
ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za
Ubunge”
Post a Comment