Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bilioni tisa kusaidia wachimbaji wadogo wadogo


Geita 9bd51 Serikali imetenga Sh.bilioni 9.8 kwa ajili ya mikopo ya vifaa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuboresha uchimbaji wao na watakopeshwa kupitia vikundi watakavyojiunga na itakuwa mkopo endelevu ili kuinua sekta hiyo ya madini kupitia wachimbaji hao.


Hayo yalisemwa leo na Kamishna wa madini wa kanda ya kaskazini Eng.Benjamini Mchwampaka wakati wa mahojiano na waaandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko mkoani arusha.

Alisema kuwa kupitia mikopo hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa wachimbaji hao kupata vifaaa hivyo ili kuweza kuinua uchimbaji wao na kuwa wa kisasa zaidi ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini ambapo hivi sasa wamekuwa wakikwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa hali ambayo wanachimba ila hawapati madini ya kutosha.



Ameongeza kuwa wachimbaji wadogo wa kanda ya kaskazini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika uzalishaji madini ikiwemo kutokuwa na vifaa vya uchimbnaji vya kisasa ,bei kubwa ya milipuko na elimu ndogo ya uchimbaji madini hayo hali ambayo inakwamisha jitihada zao za kuchimba madini hayo na kuwarudisha nyuma katika kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa hivi sasa wachimbaji wadogo walio wengi wanachimba kwa mazoea na vifaa duni ambapo elimu ya utambuzi madini sehemu yalipo ni ndogo hali ambayo inasababisha kutopata madini yakutosha na kutumia gharama kubwa zaidi.

Eng.Mchwampaka alisema kuwa katika kanda hii wachimbaji wamekuwa wakichimba kiholela bila lessen hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na hata kusababisha kifo na madhara mbalimbali ambapo maeneo hayo yanachimbwa kwa kesi sana hali ambayo ni hatari kwa badala yake wachimbaji wafate taratibu za kuchimba eneo tengefu kwa madini kwa maendeleo yao na usalama wa maisha yao kuepuka kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Aidha aliongeza kuwa hivi sasa ofisi ya kanda imejiwekea mkakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma karibu na wachimbaji katika kanda hii hususan kutoa elimu ,ya uchimbaji wa madini kitaalamu zaidi,hali ya masoko ,afya migodini ,ajira na kutoa mafunzo kwa vitendo ya namna ya ulipuaji mogodini sambamba na watatoa fursa ya namna ya uchimbaji salama na wenye tija na maendeleo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Eng.Mchwampakka alisema kuwa hivi sasa wako kwenye mchakato wa kuandaa maonyesho ya vito ,na madini mbalimbali yatakayofanyika oktoba 28hadi 30 mwaka huu mkoani hapa ambapo watahiusisha wafanyabiashara wote ncnini na nchi jirani ikiwemo Kenya ,DRC kongo ,Zambia ,Madagascar,Malawi ,Ethiopia ,Afrika ya kusini na Msumbiji ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuweza kuongeza ushindani katika sekta ya madini nchini. Chanzo: www.fullshangweblog.co,
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top