KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA YOSEFU MFANYAKAZI PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, TAREHE 5 MEI, 2013.
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la
Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko
uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia
ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.
Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika
kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti,
jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada
ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa
Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo
Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo
Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na
zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa
akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye
ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo
baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo
ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia
ovyo.
Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki duniaambapo REGINA LONGINO
KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkaziwa Olasiti alifariki dunia
siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katikaHospitali ya Mount Meru na
majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku
wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha, watu 59 wamejeruhiwa na watatu
kati yao ni mahututi. Majeruhi 38walikimbizwa hospitali ya Mount Meru
kupatiwa matibabu. Majeruhi 16walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth
kwa Father Babu, majeruhi mmojaalipelekwa hospitali ya Selian na
majeruhi mwingine alipelekwa katikahospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini.
Natumia fursa hii kutoa pole kwawafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki,
wakazi wa Arusha na Watanzania wotekwa tukio hili la kinyama. Aidha,
nawaombea majeruhi wote wa tukio hilowapone haraka.
Mheshimiwa Spika,
Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyohawakupata
madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la PolisiMkoa wa
Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwakuongeza
idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi naUsalama ya
Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMagesa Mulongo
walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyona kuelekeza
hatua za kuchukuliwa.
Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa,Makamu wa Rais
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya
Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na InspektaJenerali wa Polisi, Said
A. Mwema walikwenda Arusha na walitembeleaeneo la tukio, waliwatembelea
majeruhi na kuelekeza hatua za ziada zakuchukuliwa.
Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huoni bomu. Uchunguzi wa
kubaini aina ya bomu lililotumika unaendeleakufanywa na Jeshi la Polisi
na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi waTanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao
ni Victor Calisti Ambrose mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,
mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha ambayeanatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo.
Watuhumiwa wengine watanowaliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na
Mtanzania mmoja ambaowanashikiliwa kwa mahojiano.
Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana zawatu wachache
wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki zakidini miongoni
mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongonimwa watanzania, sina
shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu
yamikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikalihaitavumilia
hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na
tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizimbaya dhidi ya
taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na
nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.
Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziriwa Mambo ya Ndani ya
Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifawametoa maelekezo kwa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayariInspekta Jenerali wa Polisi
kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vinginevya Ulinzi na Usalama
wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukiohilo.
Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha
kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwawamoja kama taifa
na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukiohilo. Nchini
Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012
aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwaUbalozi wa
Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukuatatizo lile
kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali naWamarekani
wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisamisingi ya uaminifu
na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).
Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao
wanajitokezanchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha
yaWatanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na
kaulizinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki
miongonimwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za
kisheriaitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni
muhimukuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu
waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.
Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzaniawenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote.
Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wotewaliohusika
na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwapopote walipo
na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawatakaviongozi wa kisiasa,
kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika
ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na
utulivu.
Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakativyombo vya dola
vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenyetaarifa za
kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshila Polisi.
Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa
amani katika nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Post a Comment