xxxxx
Mwandishi Wetu,
Moshi
KATIKA kuelekea
mchezo wa jana dhidi ya Flamingo FC ya Arusha, Machava FC ambo ndio mabingwa wa
ligi daraja la Tatu, mkoa wa Kilimanjaro, wamekabidhiwa vifaa vya michezo na
uongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi.
Machava FC
walikabidhiwa vifaa hivyo ambavyo ni mipira mitano na Jezi, kama sehemu ya
mchango wa Chama hicho kwa timu hiyo ambayo kwa sasa ndio inayobeba Roho ya mkoa
wa Kilimanjaro katika medani ya soka.
Akizungumza baada ya
kukabidhi vifa hivyo vilivyotolewa kwa timu hiyo na Mjumbe wa Halmashauri kuu
CCM, Jerry Silaa, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini Aluu Segamba
aliwahakikishia wapenzi wa soka mkoani hapa kuwa wako tayari kushirikiana nao
hadi mwisho wa Safari.
“Leo tunatimiza
ahadi yetu kwa wawakilishi wetu, mabingwa wa Mkoa timu ya Machava, tunaamini
kuwa timu hii kama roho ya kilimanjaro katika mchezo wa soka itafanya makubwa na
kinachotakiwa ni kuwapa sapoti inayostahili,” alisema
Segamba.
Naye Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo Abuu Masoud, baada ya kupokea msaada huo kutoka CCM,
alisema kutokana ushirikiano unaoneshwa na wadau wa soka kwa timu yao wanaahidi
kufanya vizuri katika michezo yao yote na kuwapa raha wapenzi na mashabiki wa
Machava mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande kocha
msaidizi wa machava aliwaondoa hofu mashabiki wa timu yake kuhusu hali ya Afya
ya mshambuliaji wa kutumainiwa wa klabu hiyo, Isa Kipese na kuelekea mchezo wa
jana na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni ripoti za madaktari wanaomshughulikia
mchezaji huyo.
Machava FC ambayo
inauwakilisha mkoa katika michezo ya Mabingwa wa mikoa imekuwa ikipokea sapoti
kutoka kwa wadau wa michezo mkoani hapa ambapo hivi karibuni tu Mbunge wa Moshi
Mjini, Filemon Ndesamburo na Mstahiki Meya wa Moshi, Jafary Michael walitembelea
kambi ya timu hiyo na kuchangia fedha taslimu shilingi laki
saba.
Katika hatu
nyingine chama cha Mapinduzi CCM pia imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu
ya Gillete Fc ya kata ya Kaloleni kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama
hicho za kutoa fursa nyingi za ajira kwa njia ya
michezo.


Post a Comment