* AWASHUKURU WANA IGUNGA KWA UVUMULIVU WAO, ATAKA MAENDELEO BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA
Mbunge
wa jimbo la Igunga aliyerejeshwa na mahakama kuu Dk Peter Kafumu
akizungumza na wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini humo leo
kuwashukuru wananchi na wapiga kura wake kwa kuwa naye bega kwa bega
katika matatizo hayo, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Sokoine
mjini Igunga ukiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri
kuu ya CCM Ndugu Nape Nnauye, amesema anaomba ushirikiano kwa kila mwana
Iguna bila kujali itikadi za vyama vya siasa. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA
FULLSHANGWE- IGUNGA
Mbuge
wa Jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu akihutubia mkutano wa hadhari mjini
Igunga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi NEC 

Maelefu ya wana Igunga wakiwa katika mkutano huo leo
Wananchi wa Igunga wakipmokea mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha jimboni mwake
Dk Peter Kafumu akivishwa shada la maua mara baada ya kuwasili mjini Igunga leo
NA BASHIR NKOROMO,IGUNGA
WAKATI mapokezi ya Mbunge wa Igunga Dk. Dalally Peter Kafumu yamesababisha baadhi ya shughuli kusimama, kwa hoi hoi, nderemo na
vifijo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi ilizotoa katika jimbo hilo.
Akizungumza kwenye mkutano wa
mapokezi ya Dk. Kafumu uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa,
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM lazima
itazitekeleza ahadi zote zilizotolewa na mbunge huyo kupitia ilani ya
Chama wakapi akigombea katika uchaguzi mdogo uliofanyika 2011 jimboni
humo.
“Baada ya mahakama kumrejeshea
Ubunge mbunge wetu, CCM inaahidi kwamba ahadi zote alizotoa mbunge wenu
zitatekelezwa kabla ya mwaka 2015. Na kwa kuwa Chadema walipunguza kasi
kwa kusimamisha mbunge wenu baada ya kumpeleka mahakamani, CCM
itaisimamia serikali ili kuhakikisha inaongeza kasi ya utekelezaji wa
ahadi hizo kufidia pale utekelezaji ulipokuwa umepungua kasi”, alisema
Nape.
Alisema, licha ya Dk. Kafumu
kusimamishwa na mahakama, CCM iliendelea kutekeleza ilani katika jimbo
la Igunga, kwa sababu ni wajibu wake kutokana na kwamba CCM ndicho chama
chenye ilani inayotelekezwa kutokana na kuvishinda vyama vyote katika
uchaguzi mkuu uliopita.
Nape alisema, moja ya miradi
ambayo Dk. Kafumu na CCM waliahidi ni ujenzi wa daraja la mto Mbutu
ambalo, alisema, sasa ujenzi wake unaendelea na yapo matumaini ya
kukamilika kama ilivyopangwa.
Alisema, ahadi zingine ni kuhusu
umeme, Barabara na afya ambavyo ni miongoni mwa mambo ambayo yapo
katika ilani ya CCM, ambayo lazima CCM iyape kipaumbele kuhakikisha
yanakamilika kuondoa au kupunguza kero za wana-Igunga.
Nape aliwataka wananachi wa
Igunga kumpokea mbunge wao kwa mikono miwili na kumpa ushirikiano katika
kutekeleza ahadi zake kwa sababu ni Mbunge ambaye wamepewa na Mungu wao
na ndiyo sababu ameweza kurejeshwa na Mahakama licha ya juhudi za
Chadema kujaribu kumkwamisha asiwatumikie.
“Hukumu ya kwanza tulishangaa,
lakini kwa sababu tuliheshimu sheria kukatulia na kukata rufani. Mungu
amekaa kati yenu wana Igunga amewarejeshea Dk. Kafumu”, alisema Nape.
Akizungumzia hali ya kisiasa
nchini, Nape aliwataka wanaigunga na Watanzania kwa jumla sasa kuwa
makini na vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini akidai baadhi vimegeuka
kuwa vyama vya vurugu na vya kigaidi badala ya kuwa vya siasa kama
ilivyokusufdiwa.
Nape aliwataka wananchi wa
Igunga kuwatenga wanaoshabikia chama chochote kinachoonekana kuwa cha
fujo na kuwa na mipango ya kigaidi.
Akizungumza kwenye mkutano huo,
Dk. Kafumu alisema, amefarijika sana kurejeshewa ubunge, akisema
anatambua kuwa yeye ndiye chaguo la ubunge kwa wana Igunga kwa kuwa
wanamtumainia katika kushirikiana nao kwenye katika kuliendeleza jimbo
lao na Tanzania kwa jumla.
Dk. Kafumu aliahidi kuendelea na
utekelezaji wa ahadi zake alizowapa wananchi wa jimbo hilo, ikiwemo
ujenzi wa dalaja katika mto Mbutu ambalo alisema kutokuwepo kwa daraja
hilo kumekuwa moja ya voikwazo vya maendeleo jimboni.
“Alipokuwa nazungumza hapa
(Nape) nimetamani kulia kama mtoto wa Mkulima (Waziri Mkuu Mizengo
Pinda), kutokana na hisia zilizoniingia kutokana na maneno aliyosema.
kwa hiyo sina mengi ya kusema zaidi ya kuwashukuru kwa kunitia moyo
nilipokuwa sipo kama mbunge wenu, maana nimekuta baadhi ya ahadi zaungu
zimeendelea kutekelezwa”, alisema Dk. Kafumu.
“Napenda niwahakikishieni kwamba
nitatekeleza ahadi zangu zote na sina shaka nitafanikiwa akwa kuwa
mmenipa moyo mkubwa kwa mapokezi mliyonipa na hivyo naamini
mtashirikiana nami kwa nguvu zaidi kutekeleza ahadi hizo”, alisema.
Mapokezi ya Dk. Kafumu ambaye
aliwasili saa nane alasirin akitokea Dodona na Nape, yalianzia kiasi cha
kilometa tano nje ya mji ambapo ulienda kwa kusindikizwa na pikipiki
zaidi ya 200 na bajaji zaidi ya 60 huku wengine wakitembea kwa miguu kwa
shamrashamra hadi Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Igumnga.
Kabla ya ubunge wake kutenguliwa
na Mahkama baada ya Chadema kwenda mahakamani, baada ya kushinda katika
uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka 2011, kufuatia aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo, Rostam Aziz kujiuzulu.



Maandamano ya pikipiki yakiongoza msafara wa Mbunge wa jimbo la Igunga Peter Kafumu na Nape Nnauye.


Post a Comment