Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHAMA cha Wasafirishaji wa Barabara, chawataka madereva kutoshiriki mgomo.

 
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa mabasi Bw. Shukuru Mlawa.(Picha na Maktaba).
 
Na Hussein Makame-MAELEZO
CHAMA cha Wafanyakazi wa Usafirishaji kwa njia ya Barabara Tanzania (TARWOTU) kimewaagiza wanachama wa chama hicho na madereva wote wanaoendesha magari ya mizigo yanayosafiri ndani na nje ya nchi, kutoshiriki katika mgomo ulioandaliwa na kamati ya madereva wa malori.
Akizungumza na na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa TARWOTU Shukuru Mlawa alisema kuwa mgomo huo si halali kwa kuwa haukufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi zilizoainishwa na sheria namba 6 ya mwaka 2004 ya mahusiano kazini.
Alisema kuwa chama hicho hakitambui na wala kuunga mkono mgomo uliopangwa kuanza Mei 10 mwaka huu kuanzia saa 12:00 asubuhi, ambao uliotangazwa hivi karibuni na kamati ya madereva wa malori na kuandikwa na gazeti la Mwananchi.

Mlawa alisema pia mgomo huo si halali kwa sababu umeitishwa kinyume na sheria, hivyo ameitaka madereva wa malori walioitisha mgomo huo kujiunga na vyaa vya wafanyakzi na kufungua matawi kwenye maeneo yao ili kupata uhalali wa kuitisha mgomo kwa mujibu wa sheria.
Alisema kundi lolote la asasi za kiraia haliwezi kuitisha mgomo nje ya eneo la mwajiri au ndani ya eneola kazi kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na huharibu utaratib wa wafanyakazi wengine ambao vyama vyao vina mikataba halali ya hali bora kazini na kuvuruga tija na mapato baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Madereva walioitisha mgomo, pamoja na mambo mengine wametaka kutekelezewa madai yao ya msingi ikiwemo kupatiwa mikataba ya hali bora za kazi na kuongezewa mishahara kwa madereva wanaosafiri ndani na nje ya nchi.
Madereva hao wanataka kulipwa Dola za Kimarekani 700 kwa siku na malipo ya muda wa kazi ya Dola za Kimarekani 30 kwa siku zinazoongezeka kwa madereva wanaovuka mipaka ya nchi mbili, na malipo ya Dola za Kimarekani 300 kwa siku 14 na malipo ya muda wa ziada wa kazi wa Dola za Kimarekani 30 kwa siku inayoongekeza.
“Tunashauri kuwa madereva kushauriana, kukubaliana na waajiri wao juu ya haki, maslahi na matakwa ya hali bora kuhusu ajira zao, pia tunawashauri wafanyakazi na waajiri wao kuhakikisha kuwa wanatekeleza na kuzingatia vyema sheria, kanuni na mahusiano kazini” alisema Mlawa.
TARWOTU inawashauri waajiri kutatua na kusuluhisha migogoro au malalamiko ya kikazi kati ya wafanyakazi na waajiri wao na kutoa elimu kwa wanachama au wafanyakazi wao juu ya sheria za kazi zinazohusiana na na ajira.
Mlawa aliwashauri madereva wanaotaka kugoma kama wana malalamiko halali wafuate taratibu na kanuni za kazi na kwamba wakumbuke kuwa vyama vya vyenye mamlaka ya kutatua matatizo ya wafanyakazi katika sehemu zao za kazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top