Na Mwandishi Wetu
WAKATI
jumla ya warembo 13 wamejitokeza kuwania taji la Redds Mid Sinza 2013
iliyopangwa kufanyika Juni 7, kwenye ukumbi wa Meeda Club, kampuni ya
Tanzania Distillers Limited (TDL), kinywaji cha Chilly Willy na kampuni ya CXC Africa zimejitokeza kudhamini mashindano ya Redds Miss Sinza 2013 yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi w Meeda Club Juni 7.
Mratibu
wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa TDL imedhamini mashindano
hayo kupitia kinywaji chake cha Dodoma Wine ambao pia mwaka jana
walidhamini mashindano hayo.
Majuto
alisema kuwa wamepata faraja kubwa mwaka huu baada ya idadi ya warembo
kuongezeka sambamba na wadhamini. Wadhamini wengine ni kampuni ya TBL
kupitia Redds Original, Clouds FM, Fredito Entertainment, Sufiani Mafoto Blog na Saluti5.
Alisema
kuwa warembo wameitikia wito katika mashindano hayo kwani wanataka
kutwaa taji la Miss Redds Miss Tanzania ambalo Sinza ni watetezi kupitia
mrembo wake Brigitte Alfred.
“Bado
tunahitaji warembo zaidi ili kupamba shoo yetu ambayo ni ya mwisho kwa
kanda ya Kinondoni. Pia tunawaomba wadhamini wengine kujitokeza kwani
Miss Sinza 2013 ni zaidi ya promosheni na burudani,” alisema Majuto.
Mpaka sasa warembo 13 wamejitokeza katika mashindano hayo na wapo mazoezini chini ya Miss Tanzania Top Model, Mwajabu Juma.
Post a Comment