Flaviana Mtata, akiwasha mshumaa katika kaburi la Mama yake mzazi aliyefariki katika ajali ya Mv Bukoba.
Na Mwandishi Wetu, Dar
MWANAMITINDO
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameiomba serikali kutangaza
Mei 21 ya kila mwaka kuwa siku maalum ya maombolezo ya wasiku maalum ya
maombolezo ya wahanga wa MV Bukoba.
Ajali
ya MV Bukoba ilitokea Mei 21 mwaka 1996 na kuua watu zaidi ya 1,000 na
serikali kutangaza siku tatu za maombolezo ya kutokana na kuzama kwa
meli hiyo iliyotokea kwenye Ziwa Victoria. Katika ajali hiyo, Flaviana alipoteza mama na kaka yake.
Flaviana
ambaye kwa sasa anafanya shughuli za kuonyesha mitindo nchini Marekani
na Uingereza, amekuwa mstari wa mbele kuadhimisha siku hiyo kwa kupitia
taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation.
Akizungumza
Kwa niaba ya Flaviana Matata Mkurugenzi wa Compass Communications
Company Limited Maria Sarungi Tsehai alisema pamoja na ajali hiyo kuua
watu wengi, lakini inasikitisha kuona jambo hilo kwa sasa limekuwa kama
kumbukumbu kwa wahanga wa ajali hiyo tu na si vinginevyo.
Maria
ambaye alisema hayo katika misa maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo
iliyofanyika kwenye makabuli ya Igoma, Mwanza alisema kuwa wakati
umefika sasa wa kutangaza siku ya kitaifa ya maombolezo na kwani ajali
hiyo imeacha Watanzania wakiwa na huzuni kubwa.
Alisema
kuwa wanashukuru sana kwa miaka hii miwili wamepata ushirikiano mzuri
kutoka kwa Marine Service Company Limited na kampuni ya ndege ya
Fastjet, ambapo mwaka jana walikabidhi vifaa vya kujiokolea (maboya)
500.
Post a Comment