Balozi
Ramadhan Mwinyi Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kudumu wa 12 wa Masuala ya
Wazawa, katika mchango wake kuhusu mada ya utafiti uliofanywa kuhusu
Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga uwezo Jamii ya Wafugaji katika
Afrika, Mwakilishi huyo ameeleza kwamba Jamhuri ya Muungano inajukumu la
kuwaletea maendeleo wananchi wake wote na kwamba katika hakuna jamii
itakayoachwa nyuma. Akasisitiza haja na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa
na wadau wengine kushirikiana na Serikali kufanikisha azma hiyo lakini
pia kuunga mkono hatua na maamuzi inayoyachukua kwa manufaa ya wananchi
wake na taifa kwa ujumla. Nyuma ya Balozi ni Bi. Ellen Maduhu Afisa wa
Ubalozi .
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kwamba inajukumu kubwa la
kuhakikisha kuwa mipango yake ya maendeleo endelevu inamfikia kila
mwananchi na kwamba hakuna jamii itakayo achwa nyuma.
Na kwa
sababu hiyo, Tanzania imeitaka Jumuiya ya Kimataifa na wadau wengine
kushirikiana na Serikali katika kufanikisha azma yake hiyo, lakini pia
kutambua kuwa maamuzi mbalimbali inayoyachukua yanafanyika kwa nia
njema.
Hayo
yameelezwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alipokuwa akichangia majadiliano ya
mada ya utafiti kuhusu Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga Uwezo wa
Jamii ya Wafugaji katika Afrika.
Mada
hiyo ni sehemu ya mada kadhaa zikiwa zao afya, elimu, haki za binadamu,
ujasiliamali, vijana mila na tamadu ambazo zimekuwa zikijadiliwa kwa
nyakati tofauti katika Mkutano wa Kudumu wa 12 Kuhusu Masuala ya
Wazawa. ( Forum on Indigenous Issues) Mkutano huu ambao ulianza mapema
wiki hii unafanyika chini ya usimamizi wa Baraza la Uchumi na
Maendeleo ya Jamii la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC).
Washiriki
wa mkutano huu wapatao 2000 wanatoka katika Asasi zisizo za
kiserikali wakiwamo wawakilishi kutoka baadhi ya taasisi za kifedha
kama Banki ya Dunia, Banki ya Maendeleo ya Afrika na Banki ya
Maendeleo ya Asia.
“Tunaendelea
na jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wetu ili kuhakikisha
kwamba hakuna jamii inayoachwa nyuma kama ambavyo imeainishwa katika
Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) na kutafsriwa katika Mpango wa
Maendeleo ya Taifa na mipango migineyo” akasisitiza Balozi Mwinyi.
Hata
hivyo akasema licha ya jitihada hizo za serikali , bado kuna baadhi ya
jamii chache ambazo zenyewe zimeamua kudumisha mila, tamaduni na
maisha yao ya jadi .
Akasema jamii hizo ni zile ambazo hazifahamiki sana katika Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyo kwa jamii ya wamasaai.
Akizungumzia
masuala ya upatikanaji na ugawaji wa ardhi kwa wananchi zikiwamo
jamii ambazo mfumo wa maisha yao unategemea zaidi ardhi na mali asili
nyingine. Balozi Mwinyi amewaeleza washiriki wa mkutano huo wakiwamo
washiriki kutoka Tanzania, kwamba serikali imejiwekea sheria na
taratibu zinazosimamia ugawaji wa ardhi.
Akafafanua
kwa kueleza kwamba kwa sheria na taratibu za Tanzania, Hati ya
umiliki wa Ardhi katika ngazi ya kijiji hutolewa kwa wanajamii ambao
wanaishi au wamekusanyika katika muundo wa kijiji ambao unatambuliwa
rasmi.
“ Kwa
mujibu wa sheria zetu, ni kijiji ndicho kinatambuliwa kisheria kama
chombo huru kinachosimamia masuala ya ardhi ambapo cheti cha ardhi
hutolewa kwaajili ya matumizi ya jamii nzima”. Akasema
Na
kuongea “ Hata hivyo kuna baadhi ya maeneo hasa yale ya wawindaji
ambapo kama idadi ya jamii ile haikukidhi matakwa ya kisheria ya kuwa
na hadhi ya kijiji kutokana na uchache wao, bado kwa mfano, mwaka 2011,
serikali ilitoa hati ya kumiliki ardhi kwa ya Wahdzabe ingawa
walikosa sifa zinazotakiwa kisheria.
Akizungumza
kuhusu Loliondo ambako Serikali imetangaza kutenga eneo la kiasi cha
kilomita za mraba 2,500 za ardhi kwaajili ya makazi ya jamii ya
wamasaai na ambao wengi wao hawakuwa na ardhi na hivyo kuwa katika
mazingira magumu. Balozi amesisitiza kwamba uamuzi huo ulikuwa ni wa
manufaa kwa jamii hiyo na taifa kwa ujumla.
Akasema
kuwa eneo lililotengwa ni kubwa kuliko nchi ya Luxeburg au mara
nne ya eneo la nchi ya Singapore ambayo ina kilomita za mraba 624.
Akasema
eneo lililobaki la kilomita za mraba 1,500 Serikali imelitenga
kwaajili ya hifadhi ya wanyama pori na mazalia yake ikiwa ni pamoja na
uhifadhi wa uoto wa asili, utunzaji wa vyanzo vya maji kwa maendeleo
endelevu ya uwepo wa wanyama na kwa manufaa ya vizazi vya sasa na
vijavyo.
Naibu
Mwakilishi wa Kudumu akafafanua Zaidi kwa kueleza kwamba, uamuzi huu wa
Serikali wa kutenga ardhi kwaajili ya matumizi ya binadamu na mengine
kwa hifadhi ya maliasili ni uamuzi halali na wala haukuanza sasa bali
umekuwa ukitekelezwa katika maeneo mengi ya nchi tangu uhuru.
Post a Comment