Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni
Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by
Hilton kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za
Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo
ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi
zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira. " Taa hizi zitawasaidia
kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari
kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini
".
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph
Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya
Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na
alie kaa kushoto ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso
Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya
jua.
Mkuu wa
wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi wa
Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto) juu ya
matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa
Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa
Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman.
Toka kushoto
ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa
ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph
mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa
mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd
helman.
Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya
DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati
ya Jua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma .
Waziri wa
Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani
Afrika hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo) kila mmoja akitaka ampe
mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi taa za nishati ya jua
kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Wanafunzi
toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula na
wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya kukabidhiwa taa
zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by
Hilton.
Wanafunzi
hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata
kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na
kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya
kusomea.
Naye
Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata
amesema
"tumeamua
kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani zenye
kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila
mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha
umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao
wajitokeze".
Picha na
habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com
Post a Comment