Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akizungumza
na wasomi wa vyuo vikuu Iringa ambao ni makada wa CCM katika hafla ya
kuwaaga leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ,wa kwanza kulia ni
kamanda wa UV CCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ,katibu wa CCM mkoa
,kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
makada wa UV CCM wakimsikiliza Bw Slaa leo
Makada wa UV CCM wakiwa katika hafla hiyo leo
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Slaa amewataka vijana wa chama cha mapinduzi (UV CCM) kuwa mfano kwa vijana wa kuigwa na vijana wa vyama vya upinzani na kuepuka kuiga tabia za vurugu za kuchoma mataili barabrani kama ilivyo kwa wapinzani.
Slaa amesema kuwa itapendeza vijana wa UV CCM kufanya kazi za kujitolea kwa kusafisha barabara ambazo zimechafuliwa na vurugu za vyama vya upinzani badala ya kuiga tabia zao.
Akizungumza na katika mahafali ya ya wana umoja wa wana vyuo vikuu ambao ni makada wa CCM mkoa wa Iringa leo katika ukumbi wa Siasa ni kilimo , Slaa ambae alikuwa ni mgeni rasmi alisema kuwa kwa vijana wa CCM haipendezi kujiingiza katika makundi ya vurugu na badala yake wao kuwa mfano mwema kwa makundi ya vijana wa vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za kimaendeleo zaidi.
Pia alisema kuwa kati ya mambo ambayo kwa upande wake kama mjumbe wa NEC Taifa ataendelea kumkumbusha mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt Jakaya Kikwete ni pamoja na kutekeleza ahadi ya kuanzisha mkoa wa vyuo vikuu mkoani Iringa.
Alisema ahadi hiyo ambayo ilitolewa na chama atahakikisha inatekelezwa kabla ya Rais Kikwete kuondoka madarakani .
Kuhusu suala la Machinga kuendelea kuchochewa kufanya vurugu katika eneo la Mashine tatu mjini hapa Slaa alisema kuwa mbinu hiyo chafu inayotumiwa na wana siasa kwa ajili ya kujitafutia umaarufu ni mbinu chafu ambayo inapaswa kuepukwa na wana CCM na kuendelea kukemewa kwa nguvu zote kwani alisema si njia sahihi ya kufikisha ujumbe kwa serikali.
Slaa alisema suala la machinga si Iringa pekee bali hata yeye kama Meya wa Ilala jijini Dar es Salaam amekuwa akiwafukuza machinga hao katika maeneo yasiyo takiwa na kuwa iwapo machinga watafanya kazi kila mahali basi itakuwa ni vurugu kubwa na hakuna haja ya kuwa na sheria za mipango miji.
Credits: matukio daima blog
Post a Comment