Baadhi ya Maeneo walimo jeruhiwa 
wanafunzi hao na Mmoja kupatwa na Mshtuko wa Mlipuko wa Mabaki ya Mabomu
 hayo kutokana na Tatizo lake la Moyo alilonalo na hivyo kupelekea 
wanafunzi Watano kulazwa Ilembula Hospitali.
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwajulia Hali wanafunzi hao katika Hospitali ya Lutherani ya Ilembula.
 Mwanafunzi Evance Joseph[16]kidato cha 
Kwanza ambaye alikuwa akifanya Majaribio ya Kuchoma Mabaki hayo ya Bomu 
huku Mengine akiyahifadhi kwenye Tranka lake la Nguo.
 Wanafunzi wakiwa wanaendelea kufanyiwa 
Vipimo vya Mionzi ya Jua kutambua ukubwa wa Tatizo  katika Hospitali ya 
Ilembula Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.
 DC Njombe na Msafara Wake wakiwatazama Wanafunzi waliojeruhiwa na 
Mabaki ya Mabomu hayo. Mwanafunzi aliyejeruhiwa Katika maeneo Mbalimbali
 ya Mwili wake ikiwemo Miguuni.
 Hapa Mkuu wa Wilaya na Msafara wake ukiongozwa Na JWTZ Makambako.
 Msafara ukiwasili katika Shule ya Sekondari NABOTI Iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
 Wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba
 akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NABOTI Mara baada ya 
kutoka katika Hospitali ya Ilembula kuwajulia Hali wanafunzi Watano 
waliolazwa kwa Matibabu.
 Wanafunzi wa NABOTI Sekondari wakimsikiliza DC na Msafara wake.
 
Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari 
NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na 
Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na
 Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza 
kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya 
Jeshi.
 SOURCE: KALI ZA KITAA


Post a Comment