Hans Poppe
********
SIMBA SC usiku wa jana imesaini
wachezaji watatu wapya kwa mpigo, akiwemo mshambuliaji hatari wa timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Zahor Iddi Pazi ambaye msimu
uliopita alikuwa anatakiwa na Yanga SC akatimkia Azam FC.Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, mbali na Zahor anayechezea JKT Ruvu kwa mkopo akitokea Azam FC, wengine waliosajiliwa ni kipa Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar na beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar.
Poppe alisema wachezaji wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja.
Poppe amesema Simba SC wanasajili kisayansi na si kama wapinzani wao hao Yanga SC ambao wanaingia hasara ya fedha nyingi na wanacheza pata potea.
Kusajiliwa kwa watatu hao wapya,
kunafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika wanne,
baada ya Twaha Shekuwe ‘Messi’ wa Coastal Union kuwa mchezaji wa kwanza
mpya kusajiliwa katika timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini Simba SC, tayari imempoteza mchezaji mmoja, Mrisho Ngassa ambaye amesajiliwa na watani wa jadi Yanga SC. Chanzo: binzubeiry
Post a Comment