RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali
nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la
kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60
wamejeruhiwa.
Rais
Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amelazimika kukatiza
ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa
karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la
kigaidi.
Miongoni
mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais
ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la
Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni
ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh
Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Mei, 2013
Post a Comment