Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kagasheki amkingia kifua Kinana

Balozi Kagasheki  
*********
Alikuwa anajihusisha na masuala ya kusafirisha meno ya tembo baada ya meli iliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Sharaf kukamatwa nchini China ikisafirisha meno hayo.
Kagasheki alisema ni makosa kwa Kinana kutuhumiwa wakati kilichokuwa kimebebwa kwenye meli hiyo hakikuwa mali yake.

“Hivi ina maana wamiliki wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) au wale wa Precission Air ndiyo wanapaswa kutuhumiwa kwa kile kinachobebwa na abiria wao kweli?

Ndugu yangu Mchungaji Msigwa anafahamu ninamheshimu sana. Ingawa amenirushia makombora mengi sana. Lakini katika hili nadhani hata kama ni siasa nadhani ni kitu ambacho hakikubaliki kwa wastaarabu,” alisema.

Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Serikali imepanga kufanya operesheni dhidi ya majangili wa meno ya tembo.
Alisema hawatatangaza siku ya operesheni hiyo kutokana na kuwahusisha watu wengi.

Loliondo

Kuhusu mgogoro wa siku nyingi wa Loliondo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atatolea ufafanuzi suala la eneo tengefu la Loliondo wakati wowote katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti.

Alisema Serikali imeshughulikia kwa nia njema suala hilo lakini kutokana na malalamiko ya wananchi kufikishwa kwa Waziri Mkuu, wanasubiri uamuzi wake.

Loliondo kuna mvutano mkubwa kutokana na wananchi kupinga mpango wa Serikali kutwaa hekta 1,500 za mraba kutoka katika ardhi ya vijiji kama eneo tengefu.



MWANANCHI
Download Our App

2 comments

serikali ya ccm ndo zao hizo, yaani ni kulindana na kuleana hata wafanye madudu gani. kwa nchi za wenzetu, hata kagasheki angekuwa "Wanted" hii ndo serikali ya viongozi makini na wasikivu

Reply

umefika wakati muafaka kuwaweka benchi serikali nzima ya ccm, kwani wao nini basi? mbona KANU kule Kenya wansugua miguu, je, sisi watz tunashindwanini? mwaka 2015 uwe mwisho wao.Inatuuma sana tunapozidi kuwaona wezi na mafisadi wakikingiana vifua. Hao ni ngedere na nyani, maana lao moja. Kwa nchi zingine wote hao wangepata haki zao. mmm, yaani Tanzania kwa ufisadi!, Lo, tusipoamka na kuyaacha yakaendelea kutawala (sio kuongoza) ipo siku yatabeba hata wake zetu/waume zetu. Jamani watz, hebu tuyaondoe itakapotimu mwaka 2015!!!!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top