Wachezaji
25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha
Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi
yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).Kocha Kim amewaitaka
wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika
maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha
kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.
Wachezaji watano
walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya
Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid
Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.
LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi
moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Hiyo itakuwa mechi ya raundi
ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39
nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera
Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba
ikiwa na pointi 31.
Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi
hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi
22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.
African
Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa
na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44
ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani
mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu
ambapo hadi sasa inazo saba.
Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.
Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.
LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.
Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.
African Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba.
Post a Comment