Rais
Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais wa Serikali ya Mpito ya
Madagascar Mhe. Andry Rajoelina aliyewasili jioni ya leo Ijumaa Mei 3,
2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini,katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete, akiongozana na Rais huyo baada ya kumpokea.
Rais
wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili
mjini Dar Es Salaam jioni ya leo , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili.
Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es
Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi
na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa
ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.
Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali
ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na
mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu
utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini
humo.
Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa
Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
Post a Comment