Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo akitoa salamu za Serikali wakati wa
kongomano la siku mbili katika kuadhimisha siku Uhuru wa vyombo vya
habari lililofanyika leo jijini Arusha.
Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akitoa Ujumbe wa
Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ulioenda
sambamba na Kongamano la Uhuru wa vyombo vya Habari katika nchini za
Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Naura
Springs jijini Arusha.
Picha
juu na chini ni Meza kuu na washiriki wa Kongamano la Uhuru wa Habari
Duniani wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mwandishi wa
habari na Mwenyekiti wa Iringa Press Club Marehemu Daudi Mwangosi
aliyeuwawa mkoani Iringa wakati akitimiza majukumu yake ya kazi ya kila
siku.
Pichani
ni mmoja wa washiriki akionyesha bango lililokuwa na tukio la kuuwawa
kwa Mwandishi wa Daudi Mwangosi ambalo limeandikwa" HABARI NI MUHIMU
KATIKA UJENZI WA TAIFA, UKIMUUA MWANDISHI WA HABARI UMEUA DEMOKRASIA,
HAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAKO".
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 kwa Mjane wa Marehemu
Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi iliyotolewa na Umoja wa Vilabu vya
waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kumsaidia kuendesha maisha yake.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera na Mwenyekiti wa UTPC Tanzania Bw. Abubakari Karsani (kulia)
kwa pamoja wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 5 Mjane wa
Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera akizungumza na mtoto wa mwisho wa Marehemu Daudi Mwangosi mara
baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 5 kwa mjane wa marehemu.
Mgeni
rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakongwe katika tasnia ya Habari
walioshiriki katika Kongamano hilo. Kwa Hisani ya Mtaa kwa Mtaa
*******Mahmoud Ahmad Arusha
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera leo amefungua rasmi kongamano la waandishi wa Habari Tanzania pamoja nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuadhimisha ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari Duniani uliobeba kauli mbiu “USALAMA NA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAARIRI AFRIKA YA MASHARIKI”
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kaongamano hilo la waandishi wa habari liliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Naura springs amesema kuwa kongamano hili la vyombo vya Habari pamoja na wamiliki lina umuhimu kwa sababu litaifanya jamii pamoja na serikali kujua nini umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi na jamii yote.
Amesema kuwa uhuru wa vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa unajikita katika uhuru wa kutoa maoni na pamoja na uhuru wa kutoa habari hivyo katika kuelewa hilo vyombo vya habari vinatakiwa viwe vinafanya kazi zake pasipo kutegemea upande wowote ili kisije kuchochea au kuvunja amani ya nchi kama ilivyotokea miaka ya nyuma kwa nchini Rwanda na Burundi.
Aidha amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana zinazozikumba vyombo vya habari hususani vyombo vya kijamii ambapo wanakuwa na mazingira magumu ya kutafuta habari na kufanya wakati mwingine waandishi kuwa katika mazingira hatarishi kwa maisha yao pamoja na hali mbaya ya kiuchumi inayopelekea kutoweza kufanya kazi kuendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia ikiwepo kujiingiza katika mawasiliano ya mkongo wa kitaifa.
Kongamano la mwaka huu limeratibiwa na MISSA TANZANIA kwa kushirikiana na EAJA, Mfuko wa vyombo vya Habari Tanzania ( TMF), Muungano wa club za wandishi wa habari (TPC), Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania, Baraza la Habari Tanzania (MCA), Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) pamoj na kituo cha habari kwa wananchi TCIB na kudhaminiwa na Shirika la UNESCO.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akihutubia na kufungua Kongamano la Siku Mbili linaloenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.
Post a Comment