WILLIAM LUKUVI
CHIKU ABWAO
*******
Mbunge wa
Viti Maalum (Chadema) Iringa, Chiku Abwao na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi jana waligeuza Bunge
kama jukwaa la kufanyia kampeni za kuwania ubunge kwa jimbo la Isimani
kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Hali
hiyo ilifanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia wakati Abwao
akizungumza na kumtaka arudi kwenye hoja,badala ya kumshambulia Lukuvi
na kupiga kampeni, lakini Mbunge huyo alishikilia kuwaalikuwa anachangia
mjadala wa wizara kwa kujadili manyanyaso ya polisi dhidi ya wafuasi
wake.Akichangia mjadala wa
kupitisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha
2013/14, Abwao ndiye alianza kumshambulia Lukuvi baada ya kumtuhumu kuwa
alikuwa anatumia vibaya Jeshi la Polisi kwa kubambikia watu kesi.
Abwao
ambaye alitumia nafasi hiyo kuwa atawania ubunge katika jimbo hilo ili
kumng'oa Lukuvi, alisema kuwa wale wanaomuunga mkono wamekuwa katika
kipindi kigumu jimboni humo kutokana na kunyanyaswa na polisi.
"Lukuvi
amezoea kunipachika sifa kuwa mimi ni mzoefu wa kufungua baa tu, lakini
ameshindwa kuzitaja sifa zangu nyingine kuwa mimi ni mwanamke wa shoka
na ni tishio kwenye nafasi yake ya ubunge.
Pia alimtuhumu Lukuvi kwa kushindwa kupeleka maendeleo katika kipindi cha miaka 10 akiwa Mbunge wa Isimani.
"Jamani
watu wa Isimani mnajua wenyewe mmekuwa na wabunge mawaziri kwa miaka 20,
lakini maendeleo hakuna. Umeme unatoka Kidatu unapita juu ya Isimani na
pia barabara ni mbovu," aliongeza Abwao.
Naye
Lukuvi hakubaki nyuma kwani aliibuka na kumjibu Abwao kuwa maneno yake
ni sawa na ya 'mganga njaa' na aliwataka polisi wasishtushwe na maneno
ya mbunge huyo.
"Kizuri
chajiuza, kibaya chajitembeza, inakuwaje mbunge azungumzie mambo ya
Isimani katika mjadala huu wakati watu wanazungumzia masuala ya muhimu
ya Arusha," alisema Lukuvi akimaanisha suala la kulipuliwa kwa Kanisa
Katoliki huko Arusha.
"Ukiona
vyaelea ujue vimeundwa, Isimani umeikuta na utaiacha, wananchi mjionee
wabunge wa Iringa tupo wengi na kila mmoja anafahamu uwezo wake,"
alisema Lukuvi, ambaye pia alisifia polisi na kusema wale wanaowashutumu
basi wana kasoro.
:CHANZO MWNANCHI.
Post a Comment