
Alitaja majina ya watuhumiwa wote waliohusika na tukio hilo kuwa ni Bernad Yohana, Steven Thadeo, Adam Isidory, Jonh Benja na Sultan Kipensa wote wakiwa wamekiri kuhusika na uporaji huo na kumtaja mwenzao John Tesha kuwa ndiye aliyekimbia na fedha hizo.
Katika tukio jingine, wanamshikiria Eric Mbisa kwa kukutwa na pikipiki moja aina ya Fekon yenye rangi nyeusi na ina namba za usajili T 155 CHX pamoja na pingu na ametambuliwa kuhusika na matukio mbalimbali ya wizi wa pikipiki.
Alisema kuna baadhi ya pikipiki zinatumika katika uhalifu hasa aina ya Boxer kwa kuwa zina uwezo mkubwa wa kukimbia hivyo pikipiki zote za aina hiyo zitafuatiliwa na kuchukuliwa hatua zile zote zinazotumika bila ya vielelezo.
Alisema kuna baadhi ya pikipiki 300 tayari zimekamatwa na kati ya hizo 201 ni aina ya Boxer hivyo pikipiki zote aina hiyo zinatiliwa shaka kwa kuwa zinatumika katika ujambazi.
Alisema pikipiki zote zitawekwa alama kama teksi kwa ajili kugundulika na zitakapotumika kwa uhalifu iwe rahisi kujulikana.
MTANZANIA
Post a Comment