Aliyekaa wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa
Jamii Bw. Fidelisi Mboya akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil kuhusu zoezi la Uandaaji
wa Mpango kazi na Ununuzi kwa ajili ya Idara yake kama sehemu ya
maandalizi ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014 aliyekaa katikati
ni Afisa Bajeti wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo Michael
Msikila pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa
Jamii Bw. Aloyce Msika.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil akikagua
zoezi la Uandaaji wa Mpango kazi na Ununuzi wa Idara ya Magereza akiwa
katika picha ya pamoja na Maafisa Bajeti wa Idara ya Magereza ikiwa ni
maandalizi ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/2014.
Sehemu
ya Maafisa Bajeti wa Idara ya Zimamoto na Uokoaji wakipokea maelekezo
muhimu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbarak Abdulwakil aliyesimama, baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua Mpango
kazi na Ununuzi wa Idara hiyo katika kikao kazi kinachoendelea mjini
Morogoro.
Baadhi
ya Maafisa Bajeti wa Jeshi la Polisi wakipokea maelekezo muhimu kutoka
kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil
aliyesimama baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua Mpango kazi na Ununuzi
unaoandaliwa na Maafisa hao wa Bajeti ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya
utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
aliyesimama akitoa Maelekezo kwa Maafisa Bajeti wa Idara ya Utawala na
Rasilimali Watu baada ya kukagua Mpango kazi na Ununuzi wa Idara hiyo
unaondaliwa na Maafisa bajeti hao, katika kikao cha kuandaa Mpango kazi
na Ununuzi kinachotarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil
aliyesimama akikagua kazi ya Maandalizi ya Mpango Kazi wa Idara ya
Uhamiaji katika kikao cha kuandaa mpango kazi huo kinachoendelea mjini
Morogoro, anayemtazama ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara ya
Uhamiaji Piniel Mgonja wa pili kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Idara
ya Uhamiaji P. Kabale.kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Bajeti ya
Mwaka wa fedha 2013/2014. 

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil watatu
kutoka kulia waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
watendaji wakuu wa wizara hiyo, Makamishna, Maafisa Bajeti na Ugavi na
Ununuzi wa wizara hiyo wanaohudhuria kikao kazi cha kuandaa Mpango Kazi
na Ununuzi wa wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Bajeti ya
Mwaka wa fedha 2013/2014, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Mwamini Malemi na wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara ya Utawala na Rasilimali watu Lilian Mapfa.







Post a Comment