*AMTAKA AENDE MAHAKAMANI HATA KESHO
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka
wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa kuendelea
kufanya kazi katika eneo la Mashine tatu bila kufanya vurugu
zozote kwa wale wanaozuia kufanya hivyo.
Akizungumzia suala la Machinga kuendelea kunyanyasika mbunge Msigwa
amesema kuwa tayari suala hilo ameanza kulipigania bungeni kwa
waziri mwenye dhamana hivyo kamwe machinga Iringa wasikubali
kunyanyasika .
Aidha mbunge huyo amemtaka katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM)
Bw Kinana kutosubiri muda wa siku 21 alizozitoa kumfikisha
mahakamani kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kama hata kuwa tayari
kumwogopa mtu na kuwa siku zote atasimama katika ukweli katika
kupigania maslahi ya Taifa hili .Mbunge
Msigwa amesema kuwa hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika
vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika
kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa na hivyo suala la Kinana
kwenda Mahakamani si sawa ni kumtishia nyau mtu mzima.
Kwani alisema kuwa Chadema ina mawakili waliojitosheleza na kuwa
hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho vyovyote .
Mbunge wa
jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi wa jimbo
hilo jioni hii katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
Umati mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mbunge wao wa jimbo la Iringa mjini
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
CHANZO: FRANCIS GODWIN
Post a Comment