Kupitia
safari redio mtwara,Kamanda wa polisi mkoani Mtwara alisikika akitoa
tahadhari kwa wananchi wenye hasira kali dhidi ya mustakabali wa suala
la gesi na nia ya serikali kwa maendeleo ya watu wa kusini...
Licha ya
serikali kutumia gharama nyingi kuendesha kipindi cha BARAGUMU LA
MSIMBATI kupitia kituo chake cha habari cha TBC ambacho katika kipindi
hiki ni kama nyenzo ya kutoa elimu kwa wananchi wa tanzania hususani
KUSINI , wananchi hao wameonekana kutoelewa na kutokubaliana moja kwa
moja na serikali....Wananchi manispaa ya Mtwara Mikindani wameaswa
kununua mahitaji yao ya umuhim na kuweka ndani kwa siku ya leo kwani kwa
siku ya kesho huduma za kijamii zitasimama ama zisipatikane moja kwa
moja....
Kuna
uwezekano mkubwa wa maduka mbali mbali ya vyakula,masoko,usafiri wa umma
kama dala dala,boda boda na bajaji kusitisha huduma kutokana na TAMKO
la wanaharakati na wakereketwa wa gesi na mustakabali wa mtwara na
kusini ya kwamba huduma hizo kesho zisimame na watu wawe macho
kufuatilia mjadala wa hotuba ya waziri wa nishati na madini BUNGENI na
iwapo hawataona la maana kwenye hotuba hiyo basi wataamua lao la
kufanya.Wanamshangaa
RPC kukimbilia SAFARI RADIO kutoa tamko hilo kwani wao hawajapanga
kufanya vurugu za aina yoyote zaidi ya kutaka haki itendeke. Wanasema kwa kuwa serikali ya CCM imeamua kutumia ubabe basi na wao wataonesha ya upande wao kwa MASLAHI YA VIZAZI VYAO VIJAVYO
Post a Comment