Muwakilishi kutoka benki ya NMB akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika bonanza
la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports
Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye
viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha
makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja
anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.Lengo la la
bonanza hilo ilikuwa ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa kampuni
mbalimbali ili waweze kufahamiana na pia kudumisha umoja na mshikamano
miongoni mwao.
Pichani kulia ni Meneja wa bia ya
Castle Lager (TBL) kabula Nshimo akimkabidhi nahodha wa timu ya Fast Jet
kikombe kwa kuibuka washindi wa pili katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group.Baadhi ya wachezaji na washabiki wa timu ya Fast Jet wakishgalia kombe lao mara baada ya kunyakua nafasi ya washindi wa pili.
Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group,Ben Kinyaia akiwatoka wachezaji wa timu ya TBL
Mchezaji wa Fastjet aka Nafuu aka Kasuku akitoa pasi mbele ya wachezaji wa Infinity
Mchezaji wa timu ya TANESCO akimchomoka mchezaji wa timu ya Fast jet,wakati wa fainali yao iliyowakutanisha pamoja,ambapo timu ya TANESCO waliibuka kinara kwa kuifunga timu hiyo ya Fast Jet goli 1-0,na hatimaye kunyakua kombe la ushindi katika bonanza hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
Mchezaji wa Timu ya Infinity Communication akimkaba mchezaji wa timu ya Fastjet katika mashindano yaliyofanyika jana katika viwanja vya leaders
Kiungo mchezaji wa timu ya Fastjet akiokoa mpira mbele ya mchezaji wa Infinity Communication
Mlinda Mlango wa Infinity Communication akishuhudia mpiraa ukiingia nyavu kwake na kufanya timu ya Fastjet kuongoza kwa Magoli 2 kwa bila
Wadau kutoka Infinity Communication Kutoka Kushoto Mgisha Lukaza akiwa na wafanyakazi wenzake katika viwanja vya leaders kushuhudia timu yao ya Infinity Communication katika bonanza la May Day lililofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
Wadau wa Infinity wakilonga baada ya timu yao kufungwa magoli 2 kwa bila na timu ya Fastjet aka Nafuu aka Kasuku
Baada ya mpira wa miguu kuisha na kuwapata washindi,pia kulikuwepo na burudani iliyotolewa na bendi ya muziki wa dansi ya Skylight pamoja na wasanii mbalimbali kutoka THT.
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar wakisubiri kushuhudia burudani kutoka kwa Bendi ya Skylight Band.Picha na Josephat Lukaza/Michuzi
Post a Comment