Dk. Ali Mohamed Shein |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Chini ya
Kifungu cha 119 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amemteua
Bw. Jecha Salim Jecha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.Aidha
amewachagua wafuato kuwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
1 -- Balozi Omar Ramadhani Mapuri --
Mjumbe
2-- Bw. Salmin Senga Salmin -- Mjumbe
3 -- Bw. Nassor Khamis Mohammed -- Mjumbe
4 -- Bw. Ayuob Bakari Hamad --- Mjumbe
5 -- Jaji . Abdulhakim Ameir Issa --- Mjumbe
6 --- Bw. Haji Ramadhan Haji --- Mjumbe
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Aprili 2013
Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemteuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu
cha 61 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteuwa Dkt. Idris
Muslim Hija kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Uteuzi huo umeaza leo 30-4-2013
Viongozi hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya
jumamosi 4-5-2013, saa 2.30 Ikulu ya Zanzibar.Chanzo - ZanziNews.com
Post a Comment