Mtuhumiwa Simon Jumbe anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru. |
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kumnasa mtu mmoja ambaye anasadikika kuwa mkuu wa
genge la watu wanaojifanya Maafisa wa Ofisi ya TAKUKURU Mkoani
hapa.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo. |
“Tuliweka
mtego huo kutokana na kuwepo taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo
walitueleza kwamba kuna wimbi la baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwadanganya
watu kuwa wao ni maafisa na watumishi wa TAKUKURU baada ya kuweka mtego Mei 13
mwaka huu tumefanikiwa kumnasa huyu maeneo ya Kata ya Mkuyuni Wilayani
Nyamagana” alisema Akida.
Kamanda
Akida alieleza kwamba tangu mwezi April na Mei tumekuwa katika hekaheka za
kuwatafuta watu hao baada ya taarifa za kuwepo watu hao wanaojitambulisha kuwa
watumishi na wamekuwa akiwadanganya watu na kufanya kazi ambazo si za ofisi ya
Takukuru ikiwa ni zile za Taasisi zingine za
serikali.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida |
Naye
mmoja wa watu walioathirika na kutapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la James
Belindo mkazi wa Nyakato Buzuruga Wilayani Ilemela alisema kwamba alimfahamu
mtuhumiwa kwasababu alikuwa jirani yake naye mtuhumiwa alitumia mwanya huo wa
ujirani akimweleza kuwa kuna magari 12 yameletwa ofisini kwao yaani Takukuru
hivyo kuna nafasi za kazi ambazo anaweza
kumuunganishia.
James Belindo mmoja kati ya waliotapeliwa. |
Kamanda
Akida amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kundi la matapeli hao
wanaojifanya watumishi wa Takukuru ambao wamekuwa wakiidhalilisha na kuipaka
matope ofisi yake na kuharibu taswira iliyopo kwa jamii na kuwataka kufika ofisi
za Takukuru na kutotoa fedha bila utaratibu wa taasisi
hiyo.
Aidha
alisema kwamba kutokana na kuwepo kundi hilo ofisi yake imewataka wananchi
kuendelea kutoa taarifa za siri zitakazofanikisha kunaswa kwa watu hao ambao
wamekuwa wakiwadanganya kuwatafutia kazi,kuwatisha ili wawapatie fedha kunyume
na huduma zinazotolewa na ofisi za Takukuru Wilayani na
Mkoa.
ITAENDELEA.....SIMULIZI ZAIDI ZAJA.....
ITAENDELEA.....SIMULIZI ZAIDI ZAJA.....
Credits: gsengo blog
Post a Comment