katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina (Picha na Mbeya yetu)
KATIKA
Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood
iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi
huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa
ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi
9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa
Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa
tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa
jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura
mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga
wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa
bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya
usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na
kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali
kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema
kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo
haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo
baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu
yake.
Binti
huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar
Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku
akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na
masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa
simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha
mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi
wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
Naye
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema
alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti
angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule
umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa
kwenye shirika linalolipa.
Mlezi
wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume
amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza
kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya
kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka
ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida
|
Post a Comment