Benki ya NMB, imemkaribisha mshindi wa milioni 100 wa Vodacom MAHELA , Bwana Valerian Nickodemus, kwa kumfungulia akaunti na kujitolea na kumpa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha ili kumwezesha kuwa na matumizi yenye tija katika maisha yake, kupitia fedha hizo alizojishindia.
Mshindi
wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw.
Valerian Nickodemus (katikati) akifurahia 'Mahela' pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkuu
wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twisa, baada ya kukabidhiwa
fedha hizo, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mshindi
wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw.
Valerian Nickodemus (katikati) akikabidhiwa kadi yake ya NMB ATM na Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada
ya kufungua akaunti katika benki ya NMB. Kushotoni ni Mkuu wa Chapa na
Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twisa, akishuhudia.
Mshindi
wa shilingi Milioni 100 katika promosheni ya Vodacom MAHELA, Bw.
Valerian Nickodemus (katikati) akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Wateja
Binafsi wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kulia) baada ya
kufungua akaunti katika benki ya NMB. Kushoto ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano
wa Vodacom, Kelvin Twisa, akishuhudia.
Post a Comment